Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Waafrika tuache unafiki na woga, tuchukue hatua sasa kuhusu kile kinachoendelea kule mashariki mwa DRC.
Hakuna siri, Rwanda ndio kichocheo kikuu cha vita huko DRC kwa kuwaunga mkono kwa kila kitu waasi wa 23.
Kwa sasa waasi wa 23 inasemekana wamefanikiwa au wanaelekea kuchukua mji muhimu wa Goma, na kama hilo litakuwa kweli basi DRC itakwenda kugawanyika vipande viwili na mauaji kuendelea.
Kumaliza vita hii ni lazima Rwanda iwekewe vikwazo na hivi ni sehemu ya vikwazo ambavyo Rwanda inapaswa kuvikabili.
1. Kusimamishwa uanachama wa Rwanda katika jumuiya ya Afrika mashariki.
2. Kusimamishwa uanachama kwa Rwanda kwenye jumuiya zingine zote za kikanda au kihistoria.
3. Azimio la AU kuitenga Rwanda
4. Kuzuiwa kwa maafisa wa Rwanda kusafiri na kuingia nchi mbalimbali hususani za Africa, Ulaya na Marekani.
5. Kutaifishwa kwa mali za viongozi wa Rwanda katika mataifa mengine.
6. Rwanda kunyimwa mikopo na misaada ya kimataifa.
7. Azimio la UN kuitenga Rwanda kimataifa.
8. Rwanda kunyimwa ushiriki wowote katika mashindano mbalimbali ya michezo kimataifa
9. Kufungwa kwa milango ya kibiashara baina ya Rwanda na nchi zingine.
10. Viongozi wa serikali wa Rwanda kuingizwa kwenye orodha ya washtakiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.
Bila hata kupeleka askari, silaha yoyote huko DRC ili kukabiliana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, hivyo vikwazo tu vinatosha mnoo kumaliza hiyo vita.