Ni wakati muafaka sasa wa kuwatumia wanasaikolojia na wanasheria Kanisani wakati wa mafundisho ya ndoa na hata kwa waumini wote kwa ujumla

Ni wakati muafaka sasa wa kuwatumia wanasaikolojia na wanasheria Kanisani wakati wa mafundisho ya ndoa na hata kwa waumini wote kwa ujumla

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Ndugu,Jamaa na Marafiki kwa sasa kumekuwa na Wimbi kubwa la watu kukata tamaa na kuamua kukatisha maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo za kimahusiano,Ukosefu wa ajira, na mambo mengine kama hayo.

Sasa kwa kuwa watu hawa wengi ni waumini wa Madhehebu mbalimbali ni muhimu sasa kanisani kuwe na kipindi maalumu cha kutoa elimu ya saikolojia kwa watu namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Ndoa

Watu wengi huingia kwenye ndoa kwa sababu ya fasheni bila kujua huko ndani kuna changamoto nyingi sana ambazo zinahitaji akili kukabiliana nazo. Ni muhimu kanisa likaamua kuwaalika wanasaikolojia kuzungumza na wanandoa wapya. Wanasheria pia washirikishwe ili kuwajuza wajibu na haki za wanandoa kwa undani.
Ukweli ni kwamba kanisani wapo watu wenye taaluma mbalimbali lakini hawazitumii.

Kuwatumia Watu hawa kutapunguza changamoto nyingi sana ikiwamo vifo visivyokuwa na ulazima.

Ajira.
Madhehebu mbalimbali yanaweza kutumika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwatumia kutoa elimu kanisani na wakawezeshwa kwa pesa za kujikimu mfano vijana waliobobea kwenye kilimo,uvuvi,ufugaji wanaweza kutumika kutoa elimu kwa waumini ili wajikwamue kiuchumi.

Sambamba na hayo hata mikutano ya kijiji inaweza kutumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mambo mapya yanayoibuka kila siku ikiwamo ulinzi wa taarifa binafsi, Akili mnemba na mambo mengine.

Elimu kwa watoto.
Aidha kwa sasa kuna mambo mengi yanaendelea Duniani hususan masuala ya vita. Ni muhimu watoto wakafundishwa yanayoendelea duniani na athari zake iwe kanisani,shuleni hata nyumbani yatawasaidia kwa kiasi kikubwa sana.


Hitimisho.
Elimu hii itawasaidia sana waumini na wananchi kwa ujumla kujikwamua kiuchumi na kuacha kulalamika.
 
Back
Top Bottom