abdulrahim
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 408
- 286
Habari kwenu nyote!
Napenda kupongeza pande zote mbili kwa kazi nzuri ya kufikisha burudani kwa watanzania hasa wakati huu ambao sote tunakabiliwa na msongo wa mawazo ama kwa hakika burudani zenu zinatufariji saana.
Wahusika Clouds Media na Lady Jaydee nyinyi nyote kwa pamoja si vyema kuutaja muziki wetu unaovuka boda kila kukicha pasipo kutaja majina haya kwa historia ya pamoja mliyokwishaiweka hapo Awali.
Kwenye kufanya kazi kwa pamoja kutofautiana kupo na lakini mwisho wa siku ni kuangalia malengo ya pamoja. Ni wengi walitofautiana na Clouds media kuanzia Ant Virus mpaka Mh. Sugu mpaka juzi hapa tumeona Mh. Makonda lile alilolifanya likiwa ni kosa la wazi wala halikuhitaji Mahakama kusema ni kosa.
Na hayo yote yamekwisha na mnaendelea kufanya kazi kwa pamoja., Mimi si Raisi, Si waziri wala si Mtu mashuhuri. Mimi ni mtu NISIYEJULIKANA na Avatar yangu ina maana kubwa kwa jinsi nilivyo Napenda kuomba pande hizi mbili kwa kuanza na CLOUDS Media Kwa ukubwa uliokuwa nao na mara zote umekuwa ukijishusha Kwa pamoja na Judith Wambura kwa ukubwa wako na udogo wako kwa clouds media mkae na mmalize tofauti zenu muendelee kutuletea burudani zaidi..
Naamini mlipishana kwasababu ya mziki wetu hivyo mpatane kwaajili ya mziki wetu!
Nawasilisha!!