Ni Wakati Muafaka wa Clouds Media na Lady Jaydee Kumaliza tofauti zenu!

abdulrahim

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
408
Reaction score
286
Habari kwenu nyote!
Napenda kupongeza pande zote mbili kwa kazi nzuri ya kufikisha burudani kwa watanzania hasa wakati huu ambao sote tunakabiliwa na msongo wa mawazo ama kwa hakika burudani zenu zinatufariji saana.

Wahusika Clouds Media na Lady Jaydee nyinyi nyote kwa pamoja si vyema kuutaja muziki wetu unaovuka boda kila kukicha pasipo kutaja majina haya kwa historia ya pamoja mliyokwishaiweka hapo Awali.

Kwenye kufanya kazi kwa pamoja kutofautiana kupo na lakini mwisho wa siku ni kuangalia malengo ya pamoja. Ni wengi walitofautiana na Clouds media kuanzia Ant Virus mpaka Mh. Sugu mpaka juzi hapa tumeona Mh. Makonda lile alilolifanya likiwa ni kosa la wazi wala halikuhitaji Mahakama kusema ni kosa.

Na hayo yote yamekwisha na mnaendelea kufanya kazi kwa pamoja., Mimi si Raisi, Si waziri wala si Mtu mashuhuri. Mimi ni mtu NISIYEJULIKANA na Avatar yangu ina maana kubwa kwa jinsi nilivyo Napenda kuomba pande hizi mbili kwa kuanza na CLOUDS Media Kwa ukubwa uliokuwa nao na mara zote umekuwa ukijishusha Kwa pamoja na Judith Wambura kwa ukubwa wako na udogo wako kwa clouds media mkae na mmalize tofauti zenu muendelee kutuletea burudani zaidi..

Naamini mlipishana kwasababu ya mziki wetu hivyo mpatane kwaajili ya mziki wetu!

Nawasilisha!!
 
Kwa sasa clouds media ndio wanashikilia tasnia ya mziki wa tanzania. Ni vgumu sana kutoka nje ya mfumo wa clouds na ukanufaika kibiashara. Clouds media ndio wana ushawishi mkubwa kwenye kupromote kazi za wasanii kuliko media pratform yyte ile. Hio inadhihirishwa na jinsi wasanij wetu wanavon'gang'ania kuwa karbu ma watangazi wa clouds media ili atleast wapate promo au zile shows za Fiesta. Wasanii wanaamini kipimo bora kwao ni nyimbo zao kuchezwa na clouds.
Clouds wana falsafa yao kwamba No artist is bigger than "Clouds", hii ina apply hata kwa wafanyakazi wao, wengi huondoka wakidhani wao ndo wanaibeba clouds kumbe clouds ndo inawabeba wao, ie masoud, gadna, pj etc.

Sasa turudi kwa jay dee, sio take ya clouds kumfuata jay dee kumuomba alete mziki pale waucheze..that is a private media. It has its bills that they pay, no one pays for them, jay dee na management yake waenda wakae chini wayamalize, na wala hataonekana kajipendekeza sababu tunajua uwezo wake.

MANAGEMENT YA JAY DEE KAENI CHINI NA CLOUDS. NO ARTIST IS BIGGER THAN CLOUDS.

HATA WANASIASA WANALIJUA HILO NDO MAANA HAWAPENDI KUTOKEA KWENYE TBC.. WAO WANATAKA CLOUDS TU NA WAPO TAYAR HATA KUSHINDA STUDIO NA KINA KWISSA ILI MAMBO YAENDE SAWA.
 
imagine hadi mkulu na mwanae walikuwa wapenzi wa shilawadu
 
Ukimess na mawingu una rip.
 
Jay Dee wenyewe hajui kuimba, anaendesha maisha kwa kiki tu. Sasa hivi hamna promo, kabaki miguu juu zilipendwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…