maiyanga1
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,340
- 1,832
Timu ya Taifa ya mpira wa migu imekuwa inaitwa Taifa Stars kwa miaka Mingi. Kwa maoni yangu nadhani sasa ni wakati wa kubadilisha jina hilo ukizingatia kwamba halielezi chochote zaidi ya kiswanglish. Wakati huu timu inapoenda kushiriki kombe la Africa itapendeza zaidi kama itaenda na jina ambalo lina tija hata kiutalii. Mfano tukiita Tanzanite, Itakuwa inaelezea madini ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani.