Ni wakati muafaka wa kuwa na katiba mpya

Ni wakati muafaka wa kuwa na katiba mpya

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kwanza nimpongeze Mhe.Rais wa Awamu ya nne kwa hatua aliyofikia ya kutuletea Katiba Mpya. Ni wakati muafaka sisi wananchi KUDAI KATIBA MPYA.

Katiba mpya ndiyo itakuwa suluhisho la kila kitu ili nchi iendeshwe kwa UTAWALA BORA,WELEDI NA HAKI. Kwenye Katiba mpya kasoro nyingi zitarekebishwa na malalamiko ya wananchi yatapungua sana. Kwenye Katiba mpya

(1) Waziri hatakuwa Mbunge.

(2) Jaji Mkuu ataomba kazi.

(3) Inspekta jenerali wa Polisi ataomba kazi.

(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi ataiomba kazi.

(5) Mkurugenzi wa TAKUKURU ataiomba hiyo kazi.

(6) Makamishna wa Uchaguzi wataomba hizo kazi nk.

Tujifunze kwa wenzetu wa Kenya juzi hapa nafasi ya Jaji Mkuu walitangza na watu wakaomba na tayari amepatikana Jaji Mkuu.

Mwaka ujao uwe mwaka wa kumalizia vipengele vilivyobaki vya Katiba Mpya.

NAWATAKIA CHRISTMAS NJEMA NA MWAKA MPYA.
 
Hayo mambo uliyotaja yanapatikana kweli kwenye katiba inayopendekezwa au ni matamanio yako tu?
 
Katiba mpya inahitajika lakini siyo walioiacha kiporo bila kuimaliza pale bungeni, tunahitaji iliyopendekezwa na wananchi chini ya jaji Sinde Warioba, watwambie iko wapi
Pamoja na yote serikali hii haiwezi ikakuleteaa katiba mpya ile hali unaongelea ukiwa chumbani.

Ni vema kuishi dak 1, katika dunia hii ili vizazi viendelee kukumbuka kuliko miaka50 bila faida, si muda wa kutafuta katiba mpya chini ya uvungu kwa sasa, ni muda wa kila mtanzania kutoa kiapo cha kupatikana katiba mpya kwa gharama yoyotee.
 
Back
Top Bottom