MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
Trend ya Dunia inakoelekea ni wakati sasa wa Familia nyingi kuwa na Famiily Business yenye nguvu na kusimamiwa na Familia.
Kama ikibidi ni kwenda kutafuta ushauri kwa wasomali na Wahindi au Waarabu kwani wao wanaweza vipi kuwa na Biashara za Familia na wanatoboa? Sisi tuna nini hadi tushindwe kuendesha Familly Business?
Tatizo la ajira ni kubwa sana kiasi kwamba ajira zinatolewa kwa kujuana au ajira ni chache sana kwa sasa.
Watanzania wenye asili ya somal, Wahindi na Waarabu wako less affected sana na shida ya ajira kwa hapa Tanzania, hata kama wanasaka ajira ni kwa kiwango cha chini sana ukilinganisha na sisi Wazawa,
Hawa Wasomali au Wahindi wana Familly Business zao ambapo kijana huajiriwa mule na wakati mwingine huja kupewa potion kabisa, na hufanya kwa uaminifu na upendo mkubwa sana na kwa uchungu sana.
Sisi Wazawa tuna Biashara, au Familia nyingi zina Biashara ila ni kawaida kabisa kukuta Kijana anazunguka na Bahasha mtaani ilihali nyumbani Mama au Baba ana Project ambayo ingeweza kumuajiri kijana.Hatupendani, Hatuaminiani? Kwa nini hatuaminianu?
Kuna wakati nilikuwa Musoma kuna Familly Friend wetu ni Mfanya Biashara mkubwa sana ana Project za kutosha, sasa siku nimemtembelea akataka ushauri kutoka kwangu wa watoto wake kwamba wakasomee nini make walikuwa wanaenda Chuo na wengine walikuwa Secondary, nilijitahidi sana kutoa ushauri, na nilishauri wale watoto wasije kuwa watafuta ajira, kwamba watoto wasome masomo yenye uelekeo wa kile yeye anacho kifanya yaani Biashara, Ili warudi kumpa sapoti, nilishauri hadi aina za Kozi kama za Masoko, Uhasibu, Manunuzi na Ugavu, IT na sheria, Lakini nazani sikueleweka matokeo yake kuna walio enda kusomea Ualimu, wengine Maendeleo ya Jamii na kadhalika, Sasa Mzee kwa sasa Umuri umeenda na pia anaumwa Kisukari, Watoto wake wako Mikoani huko wamejiriwa, yeye yuko mwenyewe anapambana.Huwa nawaza ikitoke Mungu kamuita project zake zinaweza ishia pale,
Hebu sisi Wazawa tujaribu sasa kuwa na Program za Familia kuendeleza Biashara ili pia tupunguzie Mzigo Serikali wa kuajiri na tutuoe nafasi kwa zile Familia zisizo na Miradi wapate kazi kuliko kwenda kubanana nao kwenye ajira.
Tukiendelea na utamaduni wa kwamba Biashara ya Familia ni kuiba tu, kuna kuhujumiana sijui ikapanda ikashuka sisi ndo tutakao athirika sana.
Hebu tujifunze kutokana na makosa ya huko nyuma na tunayo yaona kila siku mitaani, pia tuifunze kwa wenzetu Wasomali, Wahindi na Waarabu, kama wao wanaweza na sisi tunaweza pia.
Kumaliza vyuo na kwenda kufanya kazi kwenye Biashara za Familia zitasaidia sana hata kupunguza Jam ya watafuta kazi. Tujaribu kabla hatuja fixiwa.

Upvote
10