Pre GE2025 Ni wakati sasa wanawake waache kuwa wapambe wa wagombea na badala yake wawe washindani katika nafasi za uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Katika kampeni nyingi za kisiasa nchini Tanzania, imekuwa kawaida kuona wanawake wakichukuliwa kama wapambe wa wagombea badala ya kuwa wagombeaji wenyewe. Wanawake wamekuwa wakipewa majukumu ya kushangilia, kupiga vigelegele, na kutoa kauli kama “umepitaaa baba,” bila kuangalia sera au kubaini nafasi yao kama viongozi.

Tatizo hili lina chimbuko lake katika mtazamo wa muda mrefu unaowafanya baadhi ya wanawake kuamini kuwa uongozi ni jukumu la wanaume. Hivyo, wanawake wamejiweka kando kama wacheza ngoma na washereheshaji, badala ya kujitosa kwenye uwanja wa uongozi.

Kupata Taarifa na Matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 pamoja na Zanzibar

Natoa wito kwa wanawake wenzangu, mama na dada, kubadilisha mtazamo huu. Ni wakati wa kutoka kwenye nafasi ya kuwa wapambe na kuwa washindani halisi katika nyanja za uongozi. Ni nyinyi mnayefahamu kwa undani changamoto na mahitaji ya jamii, na ni nyinyi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko yanayohitajika. Mna nafasi na uwezo wa kugombea na kuleta mabadiliko yenye maana.

Tusiruhusu tena nafasi zetu za kuleta mabadiliko kupotea kwa ajili ya kusherehesha wengine. Twende mbele na tuwe mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo kwa kuwa viongozi bora na wenye dira.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Kwa namna gani katika za vyama zinatoa fursa kwa wanawake kufikia 50/50 katika nafasi za uongozi

- Kuelekea 2025 - Kwanini wanawake huwa hawaoneshi nia ya kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za mitaa?
 
Katika kampeni nyingi za kisiasa nchini Tanzania, imekuwa kawaida kuona wanawake wakichukuliwa kama wapambe wa wagombea badala ya kuwa wagombeaji wenyewe. Wanawake wamekuwa wakipewa majukumu ya kushangilia, kupiga vigelegele, na kutoa kauli kama “umepitaaa baba,” bila kuangalia sera au kubaini nafasi yao kama viongozi.

Tatizo hili lina chimbuko lake katika mtazamo wa muda mrefu unaowafanya baadhi ya wanawake kuamini kuwa uongozi ni jukumu la wanaume. Hivyo, wanawake wamejiweka kando kama wacheza ngoma na washereheshaji, badala ya kujitosa kwenye uwanja wa uongozi.

Natoa wito kwa wanawake wenzangu, mama na dada, kubadilisha mtazamo huu. Ni wakati wa kutoka kwenye nafasi ya kuwa wapambe na kuwa washindani halisi katika nyanja za uongozi. Ni nyinyi mnayefahamu kwa undani changamoto na mahitaji ya jamii, na ni nyinyi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko yanayohitajika. Mna nafasi na uwezo wa kugombea na kuleta mabadiliko yenye maana.

Tusiruhusu tena nafasi zetu za kuleta mabadiliko kupotea kwa ajili ya kusherehesha wengine. Twende mbele na tuwe mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo kwa kuwa viongozi bora na wenye dira.

PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Kwa namna gani katika za vyama zinatoa fursa kwa wanawake kufikia 50/50 katika nafasi za uongozi
Kama unauwezo kama gwajima utakubeba, ila kama unategemea ubebwe kwa sababu ya jinsia subiri kudra za raisi kufia madarakani kama chura kiziwi, ila vinginevyo utashindwa kama kamala
 
Back
Top Bottom