Ni wakati sasa wawakilishi wa viwanda mbalimbali toka China kualikwa sabasaba 2025

Ni wakati sasa wawakilishi wa viwanda mbalimbali toka China kualikwa sabasaba 2025

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Naomba nimpe kibarua pia nimpongeze January Makamba, kwa uongozi safi wa wizara husika, hakika upele umepata mkunaji.

Lengo la uzi huu ni kumuomba Makamba kuwaalika wawakilishi wa viwanda vya China hapa nchini, katika sabasaba 2025, ili wawakilishi hao wafanye kazi mbalimbali ikiwemo kuwasaidia wafanyabiashara wa ngazi ya kati katika kuagiza mizigo na kununua mizigo mbalimbali katika viwanda vyao vilivyopo huko China.

Hii itasaidia sana katika kuleta uaminifu wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa kati na wauzaji halisi, kwa halisi.

Hili litasaidia hata mamlaka zetu za kikodi kupata pato halisi na stahili. Sorry nafahamu wazo hili litapingwa kwelikweli na mabwanyenye!
 
Wazo zuri lakini na sisi Watanzania tusumbue akili katika ubunifu Ili tupunguze kuagiza chinaa na wao au mataifa mengine yaje kwetu kununua na kuagiza
 
Wazo zuri lakini na sisi Watanzania tusumbue akili katika ubunifu Ili tupunguze kuagiza chinaa na wao au mataifa mengine yaje kwetu kununua na kuagiza
Tutabakia kuuza raw material kwa kipindi kirefu kidogo, kwa sababu baadhi ya teknolojia zimewekewa mipaka na kuwa siri kwa mataifa yaliyoendelea.
 
Back
Top Bottom