Ni wakati wa Diego(El Cholo) Simeone kutafuta changamoto mpya

Dkileo

Member
Joined
May 23, 2017
Posts
51
Reaction score
46
Alhamisi 6 ya mwezi MAY mwaka 2004 magazeti mengi ya ulaya yaliandika kuwa Jose Mourinho ameiambia Fc Porto kuwa ataondoka baada ya fainali ya UEFA champions league mwaka 2004. Baada ya kuifunga 3-0 monaco kwenye fainali iliyopigwa arena Auf Schalke Jose aliondoka Porto

Jose aliwahi kusema kama angetaka kazi rahisi basi angesalia Fc Porto na kuwa mungu mtu pale..Lakini amemua kuondoka ili kusaka changamoto mpya.. Mpaka sasa baada ya kuondoka Porto amezunguka katika vilabu vingine vi 4 tofauti ambavyo ni Chelsea,Inter milan,Real Madrid na Manchester united

Hata Pep Guardiola aliwahi kusema “nahitaji changamoto mpya.nataka kutumia nafasi hii kuwa kocha pale uingereza nataka kuzoea hali ya uingereza...nina miaka 44 ni wakati sahihi ..kuna ofa lakini sijasaini yeyote mpaka

sasa..nitakapopata timu mpya nitawajuza nyote”
Kuna wakati mwanadamu unafika unahitaji changamoto mpya..Kwa mfano Pep 2012 aliona wazi kuwa wachezaji wa Fc Barcelona wote tayari wameshashinda kila kitu..

Hawakuwa na laziada wanalo hitaji..Yamkini walihitaji mwalimu mpya mwenye mbinu mpya ambaye angeweza kurudisha hamu yao ya ushindani kuwa maradufu..Pep alikwenda kupumzika Marekani

Hata jose alikwisha liona jambo kama hili… Isinge wezekana kirahisi kwa timu kama Porto kuweza kurudia mafanikio ya 2004..Jose aliangalia mbali Zaidi aliona jinsi ambavyo samaki wakubwa wangeitafuna Porto msimu uliofuata kwa kuwachukua wachezaji wake imara

Baada ya msimu wa 2013-2014 niliamini Diego Simeone angeondoka Atletico Madrid..Atletico walichukua La Liga na kufika fainali ya UEFA champions league na kufungwa na Real Madrid..Kwakuwa niliona Atletico ingewachukua muda kuweza kurudi katika ubora ..

Chelsea waliwachukua Thibaut Courtois,Fellipe Luis na Diego Costa watu waliokuwa muhimu sana..

Lakini Simeone aliamua kubaki na hatimaye msimu wa 2015-2016 akafika fainali ya UEFA kwa mara ya pili japo alifungwa na hasimu wake yule yule Real madrid..Aliwasajili wachezaji imara sana kama Jan Oblack na Antoinne Grezman

Msimu huu Atletico imekuwa timu ya kawaida sana haswa ndani ya Champions league..Ilitolewa katika raundi ya makundi baada ya Chelsea na As Roma kuweza kupita kwenye kundi hilo ..Na hata waliposhushwa kuja kwenye Europa league sikuamini kama wangeweza kufika walipofika..

Hatimaye wamechukua taji
Huu ni wakati sahihi wa Diego Simeoni kutafuta changamoto mpya..Amewapa kila kitu Atletico kasoro UEFA champions league..

Ni muda wake wa kwenda kwenye vibarua vyenye pressure Zaidi na kukutana na wachezaji wakubwa Zaidi..Ni wakati wa kwenda kuifundisha Arsenal,Chelsea au hata Inter milan

Tatizo la Diego(El Cholo) ana moyo wa Atletico Madrid..sidhani kama ataondoka kirahisi
 
dah mi sisuport aondoke mwache tu abaki apige kazi maana pamoja na kuipatia timu mafanikio makubwa pia amewsaidia wachezaji wengi kutoka na kupata majina makubwa na wengine kwenda timu zngne zenye maslahi zaidi, si kila mtu anakuwa na malengo ya kutafuta changamoto mpya ilikujijengea cv kubwakubwa wengine huwa wanaridhika pale wao wanapokuwa njia za wengine kufanikiwa, sawa na mzee wenger pamoja na madhaifu yake mengi lakini ni mtu anayejivunia vojana wengi kufanikiwa kupitia yeye , napenda kumuona diego simeone akikaa sana pale atletico kama wenger alivyokaa arsenal
 
Mfumo wake unapendeza zaidi akiwa ATM, akienda kwingine mtamkataa kama mlivyomkataa Andre Villas-Boas na David Moyes
 
hapo spain penyewe kupambana na barcelona na madrid vilabu vinavyoogopeka ulaya nzima ni zaidi ya changamoto mpya atakayoenda itafuta sehemu nyingine
 
Huyu Zidane kashachukua kila kitu pale Madrid, angeenda Juve akawape mataji vilabu bingwa though inaonekana bado anaipenda sana Real Madrid.
 
Arsenal hapamfai na mpira wake wa kupaki basi, ataiharibu zaidi timu kama Mourinho anavyoiharibu Man U
 
wenger amekaa mpaka zigo la mavi limemwangukia mkuu
 
Muacheni el cholo, atletico ni sehemu sahihi zaidi kwake, anaipenda atletico, na atletico inampenda, mashabiki wanampenda.. Acha afanye kile kilichopo moyoni mwake.
 
Ni the highest paid coach, na ATM kwa assessment yao wanapata kile wanachohitaji na zaidi kutoka kwake.

Acha aendelee na kazi yake.

Natamani kuona jamaa akija kunyanyua UEFA siku moja akiwa na hao ATM.
 
Makombe ya mwisho ya Man U yameletwa chini ya Mourinho. Kwa hilo tu mpe credit.
Arsenal hapamfai na mpira wake wa kupaki basi, ataiharibu zaidi timu kama Mourinho anavyoiharibu Man U
 
Yaani unamshawishi mfalme akimbie himaya yake

Mfalme Samata akikimbia himaya yake pale Genk umeona kilichomkuta??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…