fofre
JF-Expert Member
- Nov 16, 2016
- 805
- 1,307
Habari zenu mashabiki wa Simba, Hongerezi kwa ushindi mzuri tulio upata jana.. do or die imefanya kazi.
Wakati mechi inaendelea jana na baada ya mwamba wa lusaka kufanya yake kuna vitu nilikuwa natafakari na nikaona kwa ujumla vina faida sana kwa club yetu pendwa ya simba endapo tutaamua kuvifanyia kazi.
Pamoja na kuwa na muwekezaji simba ni timu ya wanachama na ina mashabiki wengi Tanzania bara na visiwani. Simba ina project ya kujenga uwanja ambapo ni muda mrefu tulipewa taarifa kwamba utakamilika hata kwa uwanja wa mazoezi lakin hadi leo ni kimya.
Sisi kama wanachama na mashabiki wa simba mchango wetu ni upi katika ujenzi wa uwanja, Nikaona ni vizuri kama Viongozi wa simba wakiamua kutuchangisha mashabiki ili zoezi hili likamilike kwa haraka na tuwe na uwanja wetu. na hii inawezekana sana kutokana na matokeo mazuri inayopata na malengo ambayo yanaonekana.
Mchanganuo ambao niliufanya kwa juu juu nilichukulia kila mkoa uwe na mashabiki laki mbili (200,000) ukichukulia mikoa mikubwa ambayo inaweza kufikia idadi hiyo ni 26 hivyo kwa Tanzania tuchukulie mashabiki wa simba ni milioni tano na laki mbili (5,200,000). (idadi hiyo inaweza kuzidi)
Kila mshabiki kwa mwezi achangie shilingi elfu moja mia tano tu (1,500) kwa mwezi mzima tutakuwa tumechanga bilioni saba na milioni mia nane (7,800,000,000) hivyo kwa mwaka mzima miezi 12 tutakuwa tumechanga bilioni tisini na tatu na milioni mia sita (93,600,000,000) ukijumlisha na vyanzo vya mapato ya simba pamoja na fedha ya muwekezaji tutajenga uwanja mkubwa sana na kuwa moja ya viwanja vizuri Afrika, Ni uongozi wa simba kuamua kusuka au kunyoa.
Wewe kama mdau wa simba nini maoni yako..?