bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Imepita miaka karibia Mitatu tangu mkoa wa Arusha kukosa timu ya Mpira wa Miguu ligi kuu,Tangu JKT OLJORO ishuke daraja Jiji limekua halina tena timu ligi kuu
Kipindi cha Nyuma Soka la mkoa wa Arusha lilikua juu sana kulikua na Timu Kama AFC,Pallsons(Watoto wa baba askofu wakicheza kina Gulla Joshua),Merru Warriors...nk timu hizi zilikua zikitoa Upinzani Mkali kwa Timu kama Vile Yanga&Simba pindi walipokutana,Pia wapenzi wa Mpira wa miguu wa Mikoa ya Karibu na Arusha tulikua tukipata Burudani Murua hasa wakati wa weekend tukijumuika kwa pamoja kiwanja chetu pendwa cha Sheikh Amri Abeid Karume.
Arusha ni Mkoa Mkubwa wenye Rasilimali Nyingi kuanzia Rasilimali watu mpaka Rasilimali Mali na Pia kuna Wadau wakubwa wa Michezo Mbalimbali ikiwemo wa Mpira wa Miguu.Hivyo ifike Mahali Chama cha Mkoa Wa Arusha Na wadau Mbalimbali wa Kandanda kuunganisha Nguvu na Mkoa wa Arusha kupata timu Shirikishi ligi kuu tena itapendeza hata ziwe zaidi za Moja
Naimini Mkoa wa Arusha kuna Vipaji Vingi Sana vya Mpira na pia Kuna Timu Nyingi Sana zinazozalisha Vipaji Vya Mpira mfano Rolling stones
Hivyo itapendeza kama Wadau wa Mpira kwa Kushirikiana na Chama cha Soka kuweka Mipango Dhabiti na Endelevu ambayo itasaidia mkoa Wa Arusha kupata timu Wakilishi ligi Kuu
Nawasilisha...Asanteni