Ni wakati Wa Mkoa Wa Arusha kuwa Na Timu Ligi Kuu.

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Imepita miaka karibia Mitatu tangu mkoa wa Arusha kukosa timu ya Mpira wa Miguu ligi kuu,Tangu JKT OLJORO ishuke daraja Jiji limekua halina tena timu ligi kuu

Kipindi cha Nyuma Soka la mkoa wa Arusha lilikua juu sana kulikua na Timu Kama AFC,Pallsons(Watoto wa baba askofu wakicheza kina Gulla Joshua),Merru Warriors...nk timu hizi zilikua zikitoa Upinzani Mkali kwa Timu kama Vile Yanga&Simba pindi walipokutana,Pia wapenzi wa Mpira wa miguu wa Mikoa ya Karibu na Arusha tulikua tukipata Burudani Murua hasa wakati wa weekend tukijumuika kwa pamoja kiwanja chetu pendwa cha Sheikh Amri Abeid Karume.

Arusha ni Mkoa Mkubwa wenye Rasilimali Nyingi kuanzia Rasilimali watu mpaka Rasilimali Mali na Pia kuna Wadau wakubwa wa Michezo Mbalimbali ikiwemo wa Mpira wa Miguu.Hivyo ifike Mahali Chama cha Mkoa Wa Arusha Na wadau Mbalimbali wa Kandanda kuunganisha Nguvu na Mkoa wa Arusha kupata timu Shirikishi ligi kuu tena itapendeza hata ziwe zaidi za Moja

Naimini Mkoa wa Arusha kuna Vipaji Vingi Sana vya Mpira na pia Kuna Timu Nyingi Sana zinazozalisha Vipaji Vya Mpira mfano Rolling stones

Hivyo itapendeza kama Wadau wa Mpira kwa Kushirikiana na Chama cha Soka kuweka Mipango Dhabiti na Endelevu ambayo itasaidia mkoa Wa Arusha kupata timu Wakilishi ligi Kuu

Nawasilisha...Asanteni
 
Vijana achen bange na pombe kali ndipo mtapata team ligi kuu.
 
Vijana achen bange na pombe kali ndipo mtapata team ligi kuu.
acha zako mkuu Tarime hujaangalia wamechoma ekari ngap za bangi
Arusha Jiji la wastaarabu
Mipango tu ndo imekosekana hope muda sio mrefu nasi tutapata timu
 
acha zako mkuu Tarime hujaangalia wamechoma ekari ngap za bangi
Arusha Jiji la wastaarabu
Mipango tu ndo imekosekana hope muda sio mrefu nasi tutapata timu
Huo ustaarabu umeanza lini? Vibaka na wanyang'anyi tu huko.
 
Huo ustaarabu umeanza lini? Vibaka na wanyang'anyi tu huko.
unazungumzia Arusha Ya Lini Mkuu?
Mara Yako ya Mwisho kusika Uhalifu Arusha ni Lini,Huku hakuna Rat Road bana,Heshima kwa kila mtu ndo Jadi
 
unazungumzia Arusha Ya Lini Mkuu?
Mara Yako ya Mwisho kusika Uhalifu Arusha ni Lini,Huku hakuna Rat Road bana,Heshima kwa kila mtu ndo Jadi
arushaaa ....aisee machalii wanazingua bange.....sema kweli arusha timu ikiwepo ingekuwa poa Sana...
 
Tangu Lin bange ikacheza mpira...Dk mbili tu mtu anaenda kuzimua...mpira wanapiga piga tu na matusi kibao uwanjani...kwa arusha ni kitu cha kawaida sana kuona mtu anacheza huku ameficha msumari Wa inch 7
 
Itakuwa machalii siyo watu wa soka kabisaa miaka yote hiyo hamna timu ligi kuu duuh.
 
acha zako mkuu Tarime hujaangalia wamechoma ekari ngap za bangi
Arusha Jiji la wastaarabu
Mipango tu ndo imekosekana hope muda sio mrefu nasi tutapata timu
aiseee nimesoma chuo pale tengeru kamb ya chupa aiseee mkuu kuna wahun weng sana hapo arusha bangi,petrol alaf muda wa kwenda uwanjan wanautoa WAP labda mgod wa tanzanite utoke Kule simqnjiro uje uwekeze hapo kwa kununua wachezaj kutoka nje ya arushaaa
 
Tatizo la Arusha ni ARFA na ARDFA kama sasa hv wanataka waibebe AFC iende daraja la kwanza wakati haina uwezo na hawajajipanga... utaona figisu atakazopigwa JKT Oljoro
 
arushaaa ....aisee machalii wanazingua bange.....sema kweli arusha timu ikiwepo ingekuwa poa Sana...
Daa kila mtu anaongea kuhusu bange wapi hawavuti Bange karne ya leo
Wachezaji wenyewe wa timu mbalimbali wanavuta bange
 
Tangu Lin bange ikacheza mpira...Dk mbili tu mtu anaenda kuzimua...mpira wanapiga piga tu na matusi kibao uwanjani...kwa arusha ni kitu cha kawaida sana kuona mtu anacheza huku ameficha msumari Wa inch 7
Hahahaa isee umenichekesha ati msumari wa inchi 7
Wanakwambia Maparu nje nje zingua uone
 
Itakuwa machalii siyo watu wa soka kabisaa miaka yote hiyo hamna timu ligi kuu duuh.
Machalii wanakwambia ukileta uduwanzi unakula 70
Chama cha Soka tu hakijipanga kuna vipaji vingi sana arusha
Ref Dani Mrwanda,Nurdin Bakari,Amri Maftah wote wamepita Arusha
 
Machalii wanakwambia ukileta uduwanzi unakula 70
Chama cha Soka tu hakijipanga kuna vipaji vingi sana arusha
Ref Dani Mrwanda,Nurdin Bakari,Amri Maftah wote wamepita Arusha
hata hivyo inaonekana hawapendi soka hao kama ilivyo mikoa mingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…