Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Sisi tulio nje ya CCM hatufurahii kabisa kuona mtu yeyote akiteswa au kuonewa kwa sababu yeyote Ile japokuwa wapo Wana CCM wengi hufurahia kuona mateso ya watu wengine hususani kwa sababu za za kisiasa.Sisi tumejiapiza kuwa tutasema kweli daima na fitina kwetu mwiko.
Naposema ni wakati wa Sabaya na wengineo kuachiwa HURU sio kuwa nafurahishwa na matendo au tuhuma anazo tuhumiwa Sabaya hapana bali nachukizwa na Ubaguzi tunaotendewa sisi wananchi mbele ya sheria.
Sabaya na Kingai wote wawili wanatuhumiwa na jamii kutenda jinai. Haiwezekani Sabaya atenguliwe na kufunguliwa kesi huku Kingai akipandishwa cheo. Huu ni ubatili mtupu (Double standard) mteuaji ajue hivyo, Dunia ijue hivyo, Kingai mwenywe ajue hivyo na Watanganyika sio wajinga.
Na hii iwe fundisho kwetu kuwa hakuna aliye salama Mbele ya mfumo kandamizi usio jali haki uwe CCM au upinzani. Ni wakati wa kupinga dhuruma na uonevu na kudai KATIBA mpya ya wananchi. Watu wenye Akili wanao msemo kuwa mtu mmoja akitendewa jinai ni sawa na jamii yote imetendewa jinai.
Maendeleo hayana Vyamaa.