Ni wakati wa Serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma, hakuna kisingizio cha kutopandisha, uzalishaji umeongezeka

Ni wakati wa Serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma, hakuna kisingizio cha kutopandisha, uzalishaji umeongezeka

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Wanabodi hili ni bandiko la kuelezana ukweli,na kama viongozi wetu ni wakweli basi hakuna haja za kusubiri mpaka mei mosi ifike ili mishahara ya watumishi wa umma iongezwe.

Mwaka 2017 kwenye mkutano mkuu wa 33 wa ALAT jijini Dar es salaam rais JPM alisema hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wa umma sababu uzalishaji ulikuwa chini na hivyo serikali ilikuwa bado na mzigo mkubwa kuwahudumia wananchi.

Rais JPM alisisitiza kuwa wananchi wanatakiwa wahimizwe kulipa kodi na kufanya shughuli za uzalishaji ili pato la taifa liongezeke.

Hivi sasa TRA wanakusanya Tril 2 kwa mwezi ongezeko ambalo ni kama 50% ya kusanyo la bil 800 walizokuwa wanakusanya wakati wa awamu ya nne. Hivyo ni dhahiri kuwa sasa uzalishaji umeongezeka kama alivyotaka Rais JPM. Na kwa mantiki hii serikali inaouwezo wa kuongeza mishahara huku ikiwahudumia wananchi vizuri tu bila shida.

Ni aibu kubwa kwa taifa ambalo limeingia uchumi wa kati,huku mfumuko wa bei upo juu na kuna Mtanzania analipwa sh 390000 kama basic pay. Akikatwa kodi anabaki na sh 360000. Hapo mtu utaweza kuishi kwa raha?

My take; TUCTA na vyama vya upinzani viibane serikali ili iwakumbuke kupandisha mishahara watumishi wanaohangaika kwa kipato kidogo huku kila siku wanasota kuwatumikia wananchi.
 
Unazungumzia kupandisha mishahara wakati hata pesa ya kumalizia SGR tumeenda kuwaomba msaada wachina, kama tungekuwa na hiyo pesa ingeenda kumalizia SGR ili tujisifu tunatumia fedha zetu za ndani.

Hali ngumu mjomba usijipe moyo.
 
Mnajifanya mahodari na wajuzi wa kila professional! Hivi unajua kuwa kigezo cha kupandisha mishahara ni mfumko wa bei?
 
Mnajifanya mahodari na wajuzi wa kila professional! Hivi unajua kuwa kigezo cha kupandisha mishahara ni mfumko wa bei?
Duh! kudai nyongeza ya mishahara napo kunahitaji ujuzi?

Mfumuko wa bei sio kigezo? Upumbavu ni kipaji kama ulivyozaliwa nacho.
 
Unazungumzia kupandisha mishahara wakati hata pesa ya kumalizia SGR tumeenda kuwaomba msaada wachina, kama tungekuwa na hiyo pesa ingeenda kumalizia SGR ili tujisifu tunatumia fedha zetu za ndani.

Hali ngumu mjomba usijipe moyo.
Ujenzi wa Sgr ni mkopo,hauhusiki na tril mbili ambazo zinawahusu watumishi.
 
Bado hatujamaliza mamiradi yetu makubwa
 
Unazungumzia kupandisha mishahara wakati hata pesa ya kumalizia SGR tumeenda kuwaomba msaada wachina, kama tungekuwa na hiyo pesa ingeenda kumalizia SGR ili tujisifu tunatumia fedha zetu za ndani.

Hali ngumu mjomba usijipe moyo.

Na siyo kumalizia mkuu bali ni viraka viraka tu
 
Mkuu ilani ya uchaguzi iliyonadiwa ina kurasa zaidi ya 300, na zote zimejaa ahadi mpya. Sidhani kama suala la nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma litakuwa ni mojawapo ya kipaumbele chao.
 
Mkuu ilani ya uchafuzi iliyonadiwa ina kurasa zaidi ya 300, na zote zimejaa ahadi mpya. Sidhani kama suala la nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma litakuwa ni mojawapo ya kipaumbele chao.
Kuhudumia wananchi + mishahara vyote vipo kweye ilani ya Ccm.
 
Hivi kweli mkuu unataka mshahara uongezwe na miradi ya kimkakati isimame?
Watanzania inatakiwa tuwe wazalendo mambo madogo kama nyongeza za mishahara isiwe target yetu
Malengo yetu ni maisha bora ambayo kwa kiasi kikubwa tunefanikiwa na lengo kuu ni Miundo mbinu
Kumbuka huyu ni rais mzalendo mwenye roho ya huruma na upendo kwa RAIA wake
Ndio maana tutamlazinisha atawale milele
Tunajua hataki lakini tutaitisha maandamano nchi nzima mpaka katiba ibadilishwe
 
Kwa nini uwausishe vyama vya upinzani? Wewe pia unajuwa wameibiwa kura, je, umewahi kujitokeza kupaza sauti kukemea, au nawe mtendaji kata ambae ulishiriki uhalifu?
 
Duh! kudai nyongeza ya mishahara napo kunahitaji ujuzi?

Mfumuko wa bei sio kigezo? Upumbavu ni kipaji kama ulivyozaliwa nacho.
Utakaa na ujinga mpaka lini? Uliza Ofisi ya Taifa ya Takwimu au hata economist yeyote akusaidie. Mfumko wa bei ukipanda, lazima mshahara upande ili mpokea mshahara apate uwezo wa kununua bidhaa. Hii nitakupinga hata kwa Pilato maana wewe kipande hiki unaonekana mbumbumbu
 
Kwahiyo mleta mada unataka tuamini kwamba hizo trilioni mbili zimezalishwa na wafanyakazi wa Uma hivyo wanastahili nyongeza ya mshahara??
 
Back
Top Bottom