Ni wakati wa Serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma, hakuna kisingizio cha kutopandisha, uzalishaji umeongezeka

Ni kweli, lakini serikali hii inapika data sana, hivyo sio rahisi kuongeza mishahara maana makusanyo wasemayo sio ya kweli.
Sisi tunaamini mamlaka zenye kutoa data,kama wanadanganya watakuwa na makosa.

Kwa nini wadanganye? Ili wapate faida gani?
 
Hakuna kilichoongezeka hapo,ni Swaga za kisiasa tu,awamu ya nne billioni 800,zilikuwa hazihusishi,mapato ya halmashauri,mapato ya Idara za utalii,Wala mapato yatokanayo na faini mbali mbali za makosa ya jinai,
Sasa hv,jiwe na TRA yake ndio waanokusanya mapato,hakuna halmashauri inayoruhusiwa kukusanya mapato,
Pili anayetoa hizi takwimu,hawezi,kusema ukweli maana Jiwe,anataka useme kile kinachompendeza tu.
 
Sisi tunaamini mamlaka zenye kutoa data,kama wanadanganya watakuwa na makosa.

Kwa nini wadanganye? Ili wapate faida gani?

Aina ya siasa ya sasa inapelekea kusema uongo ili kuhadaa umma kuwa awamu hii inafanya vyema sana.
 
Ni kweli, lakini serikali hii inapika data sana, hivyo sio rahisi kuongeza mishahara maana makusanyo wasemayo sio ya kweli.
Mtasubiri Sana hata hilo lije kutokea. Hapa bora kusema ongeza tano.
 
TUCTA ni kama joka la kibisa.
 
Hakuna cha viongozi wala baba yakena viongozi ndipo tulikofika kama taifa hao wakilaumiwa pamoja na wengine wanaonewa tu.
 
Hizo pesa mnazopiga huko TUCTA mjue zina malipo yake hata kama sio leo ila mjue mtazeeka na kufa vifo vibaya. Karma lazima iwaandame.

Hivi hapo TUCTA mmeshindwa hata kuishitaki serikali hata kama mtashindwa kesi mahakamani basi watumishi wataamini kwamba mnapambana. Mnaona ni hasara sana kuwalipa wanasheria sio.

Hovyo kabisa. Endeleeni kugombania madaraka na kujilipa mishahara minono na malupukupu ya kutosha mkidhani nyie ni wajanja sana.
 
Nauliza,ingekuwa mimi ningedoubt kama serikali inakwama kufanya mambo yake. Lakini naona wanakomaa huku watumishi wanaumia.

Umepitia deni la taifa limepanda kwa kiasi gani ndani ya hii miaka mitano? Huko ndio siri yote iliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…