Ni wakati wa Serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma, hakuna kisingizio cha kutopandisha, uzalishaji umeongezeka

Mkuu punguza jazba, ndo maana nasema hivi viongozi waliyopo ni tatizo kubwa sana, so suluhisho pekee subiri niingie hapo TUCTA wafanyakazi mtafurahi tu
 
Uzuri wake serikali yetu makini imedhibiti sana mfumuko wa bei na mahitaji yote muhimu yameshuka sana mpaka sasa Watanzania tunajivunia jinsi huyu Rais wetu mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake alivyo fanya kazi ya kututumikia kuhakikisha maisha yanakua rahisi sana
Tatizo lipo kwa wapiga dili Yaani lazima waumie tu maana mianya imeziba kabisa
 
Hivi watu mnadai mpandishiwe mshahara kwa kazi gani hasa mnayoifanya huko maofisini zaidi ya kukaa siku nzima mkiwapiga vijembe wananchi ambao kimsingi ndio wateja wenu?, Hebu tajeni angalau wizara moja tu,🤔..ambayo watumishi wake wako makini kwenye kazi zao na kuna ufanisi?.....Hamna kitu!!,😳
 

Nimepewa taarifa kwamba serikali ina mpango wa kuwakata 10% wafanyakazi wote wa serikali kwa ajili ya kuchangia maendeleo.
 
Inauma kuona mtu hajui kitu, unamjulisha lakini anabisha na kukuita majina ya ajabu. Utapandishaje mshahara wakati mfumko wa bei upo chini? Hivi wanadhani mshahara ni kwa ajili ya nini? Angalia hata dollar bado haijafika 2400. Je wanataka iwe Sawa na wakati wa JK? Wapuuzi hao
 
Unatumia njia gani ya mlingano wa kiuchumi kupitia dollar? Inflation haitafsiri dollar ikishuka au ikipanda, waza Tena.
 
Duh! kudai nyongeza ya mishahara napo kunahitaji ujuzi?

Mfumuko wa bei sio kigezo? Upumbavu ni kipaji kama ulivyozaliwa nacho.
Mfumuko wa Bei ndio kigezo namba1.
Lengo la kupandisha mishahara ni kuendana na Hali ya upatikanaji wa bidhaa kwakuwa kazi ya mishahara ni kijikimu mahitaji muhimu matatu.
Mahitaji hayo yakipanda lazima mishahara ipande pia.
 
Nenda Somalia halafu uulize Tena maswali yako.
 
Ukisikia serikali ya awamu ya 5 imetekeleza ujue wavuja jasho ni watumishi wake katika sekta zote walitekeleza majukumu yao.Ulitaka watumishi washushe mbingu/ahera ndipo utambue mchango wao katika kuifikisha Tanzania kuingia uchumi huu wa kati chini?
Hayati Magufuli hakuwa Mungu useme alitenda miujiza ya kunena jambo litokee na likatokea kama enzi za uumbaji(Kama una amini kuwa ulifanyika).
 
Mimi nadhani serikali iangalie pia uwezekano wa kurejesha Bodi ya Mishahara na Maslahi ktk Utumishi wa Umma ilikuwa na umuhimu wake kama checks and balance ya kukumbusha na kushughulukia kitaalam mishahara.
 
Mimi nadhani serikali iangalie pia uwezekano wa kurejesha Bodi ya Mishahara na Maslahi ktk Utumishi wa Umma ilikuwa na umuhimu wake kama checks and balance ya kukumbusha na kushughulukia kitaalam mishahara.
Kwani ilivunjwa?
 
Jibu maswali yangu mawili, acha kuzunguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…