Katika mzunguko wa pili msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara (ikiitwa VPL) mchezo dhidi ya watani wa jadi ulizikutanisha timu hizo na matukio yasiyo ya kiuungwana yalitokea kama yalivyokea hivi karibuni. Katika mchezo huo, mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani alionekana kumtemea mate mchezaji wa Simba Asante Kwasi. Yaliongelewa mengi lakini sikumbuki kama kuna mahala Yondani alimuomba radhi mwenzie kama ilivyotokea kwa Kotei kumuomba radhi Gadiel Michael