Ni wakati wa Yondani kumuomba radhi Asante Kwasi

Kizibo255

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
515
Reaction score
376
Katika mzunguko wa pili msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara (ikiitwa VPL) mchezo dhidi ya watani wa jadi ulizikutanisha timu hizo na matukio yasiyo ya kiuungwana yalitokea kama yalivyokea hivi karibuni. Katika mchezo huo, mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani alionekana kumtemea mate mchezaji wa Simba Asante Kwasi. Yaliongelewa mengi lakini sikumbuki kama kuna mahala Yondani alimuomba radhi mwenzie kama ilivyotokea kwa Kotei kumuomba radhi Gadiel Michael
 
ni baada ya kotei kumuomba radhi gadiel Michael.. ndo mnataka yondani aombe radhi kwa kwasi?? yondani huyu huyu??
 
Bado najiuliza
Ni kwanini wadau wa michezo wamelalamika sana kwa kitendo kibaya alicho fanya Kotei dhidi ya Maiko.
Na kitendo alichokifanya Yondani dhidi ya Kwasi hakijatiliwa uzito mkubwa.
Au kwakuwa Gadiel Mauko ni Mtanzania na Kotei ni mgeni, na kama ilivyo kwa Mtanzania Yondani kwa mgeni Kwasi...!
Au kwakuwa Gadieli ni Yanga na Kotei ni Simba...!
Na Kwasi ni Simba na Yondani ni Yanga...!
Bado najiuliza.
Kwanini Yondani haombi radhi wala barua haziandikwi TFF...!
 
Mmesahau mlivyolia mpaka Yondani akafungiwa mechi kadhaa tena yule mbwatukaji wenu mpaka 'maneno ya kebehi' aliyatoa! Ikibidi John Boko naye aombe radhi kwa yule beki wa Mwadui aliyemsukumia konde la kisogoni!
 
Ndipo your ways tulivyo wanafiki
 
Mmesahau mlivyolia mpaka Yondani akafungiwa mechi kadhaa tena yule mbwatukaji wenu mpaka 'maneno ya kebehi' aliyatoa! Ikibidi John Boko naye aombe radhi kwa yule beki wa Mwadui aliyemsukumia konde la kisogoni!
Yondani hajawahi kumwomba radhi Kwasi.
Wala Yondani hajawahi kupewa adhabu yoyote kwa kosa la kumtemea makohozi kwa makusudi Asante Kwasi.
Tunataka haki sawa kwa wote, Kotei kaomba radhi wazi kabisa kwenye vyombo vya habari.
Ni wapi Yondani aliomba radhi kwa kumtemea makohozi yake machafu kwa makusudi Asante Kwasi ?
Usilete ushabiki wa timu.
Lini Yondani kaomba radhi au kuadhibiwa ?
 
Mkuu mbona ishu ya Yondani ilinyoshewa bango sana tena kuzidi hata hii ya Kotei.
 
Duu we jamaa! Ni kweli Yondani hakuomba radhi lakini alipewa adhabu na Tff labda hukufuatilia ile ishu ilivyoisha! Vipi kuhusu nahodha wenu bin Boko aliomba radhi kwa yule jamaa aliyemtwanga konde la kisogoni? Siungi mkono wachezaji watovu wa nidhamu popote walipo!
 
Kuomba radhi ni utashi wa mtu lakini kwa yondani sheria zilifuatwa na adhabu inayostahili yondani alipewa ndo tunachotaka kwa kotei hatua stahiki zichukuliwe we kijana wa manara acha kubwabwaja hapa
 
Kuomba radhi ni utashi wa mtu lakini kwa yondani sheria zilifuatwa na adhabu inayostahili yondani alipewa ndo tunachotaka kwa kotei hatua stahiki zichukuliwe we kijana wa manara acha kubwabwaja hapa
Naona Povu
Sawa umeshinda
 
Hivi James Kotei ndio ameandika kiswahili kizuri kumpita hata Gadiel! Nadhani ameandikiwa.

Vv
 
Kwanza sheria ichukue mkondo wake, huyo kotei afungiwe mechi 24 ndiyo aombe radhi, tunajua kabisa kotei hajaomba radhi bali amelishwa maneno na wahuni akina manara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…