Afrika_Bora
Member
- Oct 20, 2020
- 77
- 159
Kuroiler ni kuku Chotara ambae hupatikana kwa kupandishia kuku wa jamii mbili tafauti ili kupata matokeo mazuri zaidi ukilinganisha na kuku wa kawaida.
Matokeo hayo ni pamoja na kutaga mayai mengi au/na pia kuwa na miili mikubwa kwaajili ya nyama.
Hivyo kumfanya mfugaji wa kibishara kupata kipato kizuri kabisa.
Kila penye fursa huwa hapakosi upigaji. Kutokana na shuhuda mbali mbali kutoka kwa wafugaji ni kwamba ili upate faida nzuri kupitia kuku hawa, unahitajika kuwa na kuku wale wa Uzao wa kwanza (First filial generation "F1") au wanao karibiana na hawa, yaani F2.
Ikiwa na maana kila uzao unavokwenda mbele ndio matokeo mazuri kibiashara hupungua.
SWALI : Ni wapi au kampuni gani inajishuhulisha na uuzaji wa kuku aina hii ya Chotara Kuroiler ambao ni uzao wa kwanza F1 ?
Karibuni wadau tujadili na tupeane taarifa pia maarifa sahihi kwaajili ya ufugaji wa kibiashara na kujikwamua kiuchumi .