Uweri the second
Member
- Mar 11, 2021
- 35
- 31
Ndugu wanajamvi,
Nimehamasika sana na ushauri uliotolewa hivi karibuni na mh. Waziri mkuu Majaliwa kwamba sasa ni zamu ya watanzania kutajirika kupitia zao la alizeti.
Naamini huu ushauri umekuja baada ya hali ya bei ya mafuta inchini kupanda sana kwa kipindi kifupi.
Mimi ninaishi Arusha lakini nina mpango wa kuhamia Dodoma kwa shughuli zangu za kibiashara lakini pia natamani sana kuanzisha kilimo cha alizeti kutokana na hii hamasa ya mheshimiwa PM. Lakini pia kwa ukweli kwamba mafuta bado hatujitoshelezi kama inchi kwani sehemu kubwa bado tunaagiza nje.
Wadau wenye uzoefu najua humu mpo ndio maana nimekuja ili nipate mawili matatu ili kujua kama ninachokiwaza kufanyia hapo dom kinafaa au la.
Asanteni.