Ni wapi naweza kuhudhuria maonyesho ya projects za computers, apps, softwares, n.k. lengo ni kuwekeza, nipeni pia elimu na tahadhari kabla sijawekeza

Ni wapi naweza kuhudhuria maonyesho ya projects za computers, apps, softwares, n.k. lengo ni kuwekeza, nipeni pia elimu na tahadhari kabla sijawekeza

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Najua kuna vijana wengi wana mawazo yao lakini changamoto huwa ni fedha.

Ningependa kujua ni wapi naweza kupata fursa ya kuweza kuhudhuria maonyesho ya projects zinazodeal na mambo ya computers, simu, apps, n.k.

Kwa sasa nipo Njombe, huku ni bila bila. sehemu ya karibu nayohisi kuna hayo mambo ni Mbeya kwasababu ni mkoa wenye vyuo vingi sana nyuma ya Dsm, lakini pia naweza kwenda Dar kwasababu nasikia kuna kambi nyingi za mambo haya na vyuo vipo vingi zaidi pamoja na watu wenye passion kwenye hii sekta

Budget yangu nindogo, initial investment ya kuingia mkataba, ni milioni 2, kisha baada ya hapo tuwe tunagawana 50 / 50,

  • Sehemu zipi niende
  • njia nzuri ya ku aproach vijana wenye mawazo
  • tahadhari za kuchukua
  • n.k,
 
Inasikitisha sana kuona nyuzi muhimu kama hizi watu njwiii wamelala, lakini zikianzishwa nyuzi za kunjunjana uzi una trend
 
Hapo utafeli badala yake Nakushauri Tafta idea Mfano unaweza kutengenezewa App ya Kilimo kuwakutanisha wakulima na Wanunuaji ukawa unacharge Ada ya Subscription au in App purchase...Unaweza kutengeneza B2B Ecommerce App...aisee idea zipo nyingi mno

Binafsi ni mjuzi wa hiyo field mwaka wa 6 sasa nauelewa vizuri unaweza pitia Nyuzi zangu kisha Njoo na hiyo Bajeti nikutengenezee kitu roho inapenda

[2/24, 00:30] Je, App ya Biashara ya Vipuri Kama BeForward kwa Soko la Tanzania Itafanikiwa au ni Kupoteza Muda?

Kwasasa App zote zinapatika Playstore pakua na Andika maoni yako.

Je, nastahili pongezi kwa haya niliyofanya?
 
Kwa Tanzania sina uhakika, kwa kimataifa mojawapo hii inaitwa "Consumer Electronic Show (CES)", ni show kubwa Sana ya technolojia....hufanyika kila mwaka.
Mwaka huu Consumer Electronic Show (CES) 2025 ilifanyika Las Vegas nchini Marekani.
Lakini pia hata Huawei wanayo event yao inayofanyika kila mwaka na developers kutoka maeneo mbalimbali duniani wanaalikwa kwa ajili kupata elimu na kujifunza kuhusu software, NK.
 
Chief-Mkwawa hivi 16gb ddr4 ram ya laptop bei gani na naweza kupata wapi mpya. Maana naona laptop yangu kila saa inaniletea blue screen of deatg yenye stopcode ya memory management. Nimeupdate drivers, nmeipga windows mara 3 mwisho nikasoma mtandaoni kuwa mara nyingi ni ram
 
HIZI NI BEI ZA RAM

4GB DDR3 ZA LAPTOP NA DESKTOP 12,000
4GB DDR3L ZA LAPTOP NA DESKTOP 13,000
2GB DDR3 ZA DESKTOP 10600MHZ 13,000
4GB DDR3 ZA DESKTOP 10600MHZ 20,000
4GB DDR3 ZA work station bei 20,000
4gb ddr4 ya z400 bei 25,000
4gb ddr4 za laptop na desktop 2400t/2666mhz 20,000

8gb ddr3 ya desktopna laptop bei 27,000
8gb ddr3l ya desktop na desktop bei 30,000

8gb ddr4 ya desktop na laptop bei 37,000

16gb ddr4 ya laptop na desktop bei 75,000

16gb ddr4 ya desktop bei 140,000

kuweka order whatsApp/call 0617833822

mikoani tunatuma
 
Jaribu kutoka hiyo ram alafu uifute na ufuto wa penseli usafishe na hiyo njia ya ram alafu irudishe
 
HIZI NI BEI ZA RAM

4GB DDR3 ZA LAPTOP NA DESKTOP 12,000
4GB DDR3L ZA LAPTOP NA DESKTOP 13,000
2GB DDR3 ZA DESKTOP 10600MHZ 13,000
4GB DDR3 ZA DESKTOP 10600MHZ 20,000
4GB DDR3 ZA work station bei 20,000
4gb ddr4 ya z400 bei 25,000
4gb ddr4 za laptop na desktop 2400t/2666mhz 20,000

8gb ddr3 ya desktopna laptop bei 27,000
8gb ddr3l ya desktop na desktop bei 30,000

8gb ddr4 ya desktop na laptop bei 37,000

16gb ddr4 ya laptop na desktop bei 75,000

16gb ddr4 ya desktop bei 140,000

kuweka order whatsApp/call 0617833822

mikoani tunatuma
16gb ddr4 ya laptop na desktop bei 75,000

16gb ddr4 ya desktop bei 140,000
Hapa sijakuelewa naona bei inatofautina. Na zinakuwa brand new au used
 
16gb ddr4 ya laptop na desktop bei 75,000

16gb ddr4 ya desktop bei 140,000
Hapa sijakuelewa naona bei inatofautina. Na zinakuwa brand new au used
Hao jamaa walinitumia tangazo tu cheki nao wako kariakoo nenda dukani kwao ukajionee
 
Najua kuna vijana wengi wana mawazo yao lakini changamoto huwa ni fedha.

Ningependa kujua ni wapi naweza kupata fursa ya kuweza kuhudhuria maonyesho ya projects zinazodeal na mambo ya computers, simu, apps, n.k.

Kwa sasa nipo Njombe, huku ni bila bila. sehemu ya karibu nayohisi kuna hayo mambo ni Mbeya kwasababu ni mkoa wenye vyuo vingi sana nyuma ya Dsm, lakini pia naweza kwenda Dar kwasababu nasikia kuna kambi nyingi za mambo haya na vyuo vipo vingi zaidi pamoja na watu wenye passion kwenye hii sekta

Budget yangu nindogo, initial investment ya kuingia mkataba, ni milioni 2, kisha baada ya hapo tuwe tunagawana 50 / 50,

  • Sehemu zipi niende
  • njia nzuri ya ku aproach vijana wenye mawazo
  • tahadhari za kuchukua
  • n.k,
Ningekupa share kwenye hii project yangu ila 2M then fifute fifute it means unataka uwe investor pekee kwenye hiyo startup kwa maana baada ya wewe hakuna share zitakazouzwa tena, sasa kwa hiyo million mbili mnatakiwa muajiri mpate na sehemu ya makutano ambayo lazima mtailipia Kodi, mtawezaje kusavaivu?
 
Chief-Mkwawa hivi 16gb ddr4 ram ya laptop bei gani na naweza kupata wapi mpya. Maana naona laptop yangu kila saa inaniletea blue screen of deatg yenye stopcode ya memory management. Nimeupdate drivers, nmeipga windows mara 3 mwisho nikasoma mtandaoni kuwa mara nyingi ni ram
Jamaa naona kakujibu, bei nzuri almost zinafanana na online,

Sema memory management ni either ram ama Storage kimoja wapo, sometime kama hdd/ssd imelegea na inacheza ama inaharibika inaweza kuleta hilo tatizo,

Ungeweka screenshot ama error code tungejua zaidi.
 
Hongera mkuu kwa wazo zuri na utayari wa kuwezesha vijana wasonge mbele. Kwenye haya mambo hasa ya tech ideas, binafsi sio mgeni na nimepata vihela hapa na pale vya ruzuku. Cha msingi hasa kwako kama mwekezaji ni usiweke hela yote kwenye idea au kampuni moja. Kwa takwimu za hapa ndani na duniani, tech ideas zinakufa sana, zaidi ya 90%. Sababu ni nyingi ila ndo uhalisia from stories and personal experience. Sasa ufanyeje? Tafuta vijana ambao tayari wameanzisha jambo lao, wanatembea, nguvu zao zinalipa nauli angalau ila wakupata nguvu ya hela, watapaa. Hapa ndo pa kuwekeza.

Changamoto hasa kwa nchi zetu hizi ni vijana wasomi ni wengi, ajira hamna, na pia wazuri wa ujuzi wapo na ni wachache, ila hawajapata pa kujishkisha. Sasa akipata kihela kidogo, anakuwa na mihemko na wakati mwingine anakuwa na tamaa ya kuvaa, kula vizuri na kusahau biashara/idea yake. Hivyo hela inaishia kusiko. So kuwa makini na mambo kama haya. Pia kumbuka hela ya nje haitumiki kuanzisha biashara, ni ya kuendeleza.

Ideas ni nyingi sana na ambazo ni zuri zipo pia. Zinahitaji validation, yaani kufanyiwa tathmini kuhakikisha zinaweza kuwa biashara. Kama upo tayari unaweza kuwekeza kwenye hatua hii ya awali, ila haina uhakika wa kurudi. Kwa ujumla, wangepatikana wengine ambao wana hela zao ambazo zikipotea hawatalala njaa, ingesaidia sana kuhakiki na kusimamisha mawazo bora au biashara changa ambazo zinakufa sababu ya vitu vichache.

Kama mdau alivyosema hapo awali, Buni/COSTECH ambapo ni DSM, kwa Mbeya/Iringa cheki Kiota Innovation Hub, Mbeya Startup Community, RLabs.

Karibu sana
 
Back
Top Bottom