Mkuu hii kitu ndo my next investment ( day care au nursery) ni project ninayo iwaza sana. Nipe uzoefu kidogo,,, like how you started,,, changamoto za mwanzo na uliwezaje kupata watoto,,, thank you in advance
Asante mkuu,,
Nilifungua kituo tarehe 2/11/2020
Kwa kweli nilianza na mazingira magumu kidogo,,kwani nilikuwa sina kabisa mtaji,kwaiyo kutokana na mazingira kuwa kidogo hayavutii,,niliamua kuweka kiasi kidogo cha ada lengo ni kuwavutia wazazi wengi,,
Asante MUngu nilifanikiwa,,siku ya kwanza nilipata watoto wawili,,nilianza nao ivo ivo.
NB:sikuwa na ujuzi wa hii fani,,elimu yangu ni form six.
Nimeendelea ivo kufika december 2020,nikawa na watoto kama kumi na tano,,nimeenda nao hadi mwishoni mwa december 2020.
January 2021,Mungu alinisaidia nikapata watoto wengi kidogo ,,kama 40+
Nimeendelea kufikia may 2021,nilikuwa na watoto 80+
Sasa changamoto ikawa ni class management,,kwa sababu nilikuwa peke yangu,,nikawa naenda ivo ivo,,
Sasa hapo nikaongeza ada kidogo ,,
Lakini ada hiyo wameanza kulipa kuanzia january 2022,,
January 2022,nimeanza na watoto50+ na hadi sasa nina watoto 60+ ila nimefunga kupokea new intake Kutokana na kwamba class management inakuwa ngumu kidogo ,,na nina darasa moja tu kubwa that is why nashindwa kuongeza mwalimu,
Changamoto ni nyingi pia ,,nitaziandika hapa,