Habari za asubuhi wanajukwaa. Nahitaji kumwanzishia biashara ya vitafunwa mdogo wangu ili kumwepusha na vijiwe vya kijinga huku akisubiria tokeo la form 4... Moja ya mahitaji ya hii biashara ni container, sasa Kuna yale masanduku maarufu sana jijini Dar es salaam, mara nyingi hutumiwa na madogo ambao wanauza samosa/Sambusa mtaani. mwonekano wake yameundwa kwa bati za aluminium na vioo ili kuonyesha bidhaa iliyopo ndani. Kwa anayefahamu ni wapi naweza kuyapata nangojea Comments