Ni wapi nitapata mwanamke wa kuoa?

Mkuu, jamaa ameulizia location bana....wapi mke anapatikana?
Mjibu hivi: tampata shuleni kama anataka mwalimu.....au anaweza akajikuta anaibuka na MEM au MES.
Kamanda umeadimika kweli ndo mambo ya kusaka jiko nini?
Nakushauri ukamate Mwalimu wa shule ya Msingi au wa O'Level
 

Isije kuwa unatafuta mtakatifu. Hao hawapo. Binadamu wote tuna udhaifu. Ili mradi wewe ni binadamu si rais kuishi na mtakatifu kama mkeo.
 
kaka kama vp anza na bebii huyo, si unaona alivyoizimikia thread,, dada bebii mwaga swaga zako za cv kabla wavaa cl hawajamuwai
ahaa wapi single but not reachable hapa weeeeeeeeeeeee
 
Ila tambua kitu kimoja ni ngumu sana kumpata mwanamke aliyetimiza vigezo vyote unavyovitafuta,kila mtu anamapungufu yake,ambayo hata ww unayo lkn kibinadamu inabidi baadhi ya mambo tuvumiliane, cha msingi angalia yale yaliyo muhimu km tabia,vitu ambavyo havirekebishiki,lkn vitu km elimu,mwonekano na vingine vidogovidogo ambavyo vinatengenezeka usivijali sn,mungu atakusaidia utampata aliye wako.
 
Isije kuwa unatafuta mtakatifu. Hao hawapo. Binadamu wote tuna udhaifu. Ili mradi wewe ni binadamu si rais kuishi na mtakatifu kama mkeo.
siina maana hiyo kaka, ndio mana nikasema hata robo, nafahamu kabisa ya kwamba hakuna binadamu aliyekamilika na nipo tayari kukubali yale mapungufu madogo madogo na ambayo yanaweza kurekebishika
 

Gudboy,
Kwanza kabisa, mshirikishe Mungu katika utafutaji wako, atakuletea yule ambaye moyo wako umempenda. Kwangu mimi, inapendeza zaidi kama huyo umtakaye, mwanzie kwenye urafiki, then hiyo itakusaidia wewe kumjua vizuri.
Pili, Kama unamtafuta the perfect one, kwa kweli sio rahisi kumpata. Inawezekana vigezo na masharti yako ni magumu sana. Ila unaweza ukampata mahali popote tu............All the best.

Stay blessed.
 
Reactions: BAK
sasa wewe unataka tu kuletewa mke ina maana hata sifa za umtakae hujui sio.
Huyu gudi boi bure kabisaaa. anaona watu wanaulizia mara mbili mbili vigezo,labda watu wajipime.. hajui kama ndo responc za kiutu uzima zenyewe?...lol... safi mwaya ,, dada Bebii
 
mke unaweza ukampata maendeo haya tandale, manzese,buguruni,m/nyamala,kigogo, mburahati .........
 
ni kweli kaka, hili jambo kwa vijana wa sasa ni gumu mno. huwa nawaambia watu sisi ambao bado hatujaoa tuna maisha magumu sana, lakini ukiangalia ni kweli, kumpata tu wa kuoa ni shughuli pevu
Kumbe tupo wengi tunaotafuta wachumba wa kuoa!? Nina mwaka wa tatu bado sijampata wa kuoa...wote wana tabia moja ninayoichukia sana ya kusema uongo.
Nikishagundua mchumba kaniongopea ktk mazungumzo yetu, basi uhusiano wetu huwa unaishia hapo. Kwani naamini atanidanganya mengi kwenye maisha yetu ya ndoa.
 
Kikubwa mdogo wangu mwombe mungu umpate mke mwenye hofu ya mungu haijalishi eneo
 
Mtangulize mwenyezi mungu kwenye kila jambo lako na utafanikisha malengo yako...
 

ngoja niendelee kufuatilia huu mjadala una msaada mkubwa sana kwangu .wakuu tunasaidieni sie mabachelor (kimawazo, mbinu , uchaguzi na sifa maana unaweza ukawa unamuimagine mke kwa vigezo vyako unaweza ukajikuta unaambulia patupu)maana hii kitu ni CHANGAMOTO sana . mfano wengine nature ya kazi unayofanya unakuta interaction na wadada nayo ni ngumu. unaweza ukawa unatafuta vigezo vya kawaida tu,
mungu nisaidie ni pate mkwe mwema amina
nawasilisha..
 

mkuu inawezakena una udhaifu katika suala zima la kutafuta kitu unachohitaji , elewa kwamba
  1. kuna vitu unatakiwa wewe kama wewe uvione kwa mwenza unayemfikiria
  2. kuna mambo ambayo ni vigumu kuvipata kwa siku moja ila unatakiwa umweke karibu kwani jinsi anavyokuwa karibu anapoteza nguvu asili ya kuficha kitu
  3. wewe yawezekana una haraka sana ya kufikia malengo yako
  4. mfanye mtu unayetarajia kama rafiki yako wa karibu
  5. usiwe mwenye misimamo na imani zako zinavyokusukuma iwe na ndiyo iwe
 
mkuu msaada tafadhali kwani muda sahihi ni upi wa kuwa na mweza? Na atleast ni ukae muda gani kama kuwa wachumba mpate faragha ya kufahamiana .
 
mkuu msaada tafadhali kwani muda sahihi ni upi wa kuwa na mweza? Na atleast ni ukae muda gani kama kuwa wachumba mpate faragha ya kufahamiana .

hakuna muda maalumu ambayo unaweza kuwa umepangiwa ila inategemea na wewe nini hasa lengo la awali , aslimia kubwa hukimbilia kumvua chupi mwanamke kwa kudhani ndo ataweza kumjua zaidi lakini ukweli unaweza kuwa nae karibu kama rafiki wa kawaida ukapata nafasi ya kuelewa tabiazake zikoje au ni mtu wa aina gani ila naamini utakuwa na ABCDE... na nini unakitaka
 

mkuu kuna mambo amabayo hayatakiwi au hayahitaji haraka kuyafahamu kutoka kwa mwanamke kwani katika kumdodosa unamlazimisha akudanganye
 
mkuu kuna mambo amabayo hayatakiwi au hayahitaji haraka kuyafahamu kutoka kwa mwanamke kwani katika kumdodosa unamlazimisha akudanganye
hivi ni tatizo hapa ni style ya kumdodosa ndio ambayo inamfanya akudanganye/ au kuna jingine tafadhali msaada...
Maana hamnakitu na chukia kama kudanganywa inaiuma sana nikigundua hili...
 
hivi ni tatizo hapa ni style ya kumdodosa ndio ambayo inamfanya akudanganye/ au kuna jingine tafadhali msaada...
Maana hamnakitu na chukia kama kudanganywa inaiuma sana nikigundua hili...

tatizo ni wewe jinsi ambavyo utakaa na kumuuliza ndo maana nikasma kuna mengine yakupasa usiwahi kuuliza
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
daladala
kanisani
kazini
mtaami
chuo
harusi
au sherehe yeyote
club
msibani
anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf

Bebii hata jf hahahaahaaahaaaaaa mwonee huruma kijana huyu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…