Ni wapi Tanzania kuna mfumo wa unenepeshaji (Feedlot Experts)

Ni wapi Tanzania kuna mfumo wa unenepeshaji mifugo (hasa wa nyama)kwa njia ya "feedlots" sijui neno sawia kwa kiswahili. Kama Kuna wadau wanazo hizo Center tusaidiane ili nijifunze jinsi ya kuanzisha na kuendesha feedlots.

Nimetembea mashamba mengi ya serikali ila sijaona hii kitu. Huenda haiko profitable kwa mazingira ya hapa kwetu.
 
kipind cha nyuma wakat nasoma, Tuliwah kwenda kongwa ranch, Tulikaa pale miez miwil na walikua wanafanya wananenepesha wanyama.
Kile walikua wakifanya walikua wananunua ngombe ambazo zina umri wa mwaka mmoja au karibia mwaka mmoja then wanawapiga lishe wanachunga wakirud wanapewa lishe nzur na walikua na chumv zao wanapewa.
Haikua full feedlot maana hawakua wakipatiwa concentrates but Hay na makoro koro mengine.
Sijajua mpaka sasa kama ranch ile wanaendelea na mfumo ule. maana ilikua mwaka 2014
 
Nadhani yoyote anayeweza kufuga / anayefuga hivyo anajua kunenepesha na anaweza kunenepesha... (unaweza kuchukua elimu kutoka kwao)

Tofauti ya wafugaji wengine wanaozalisha wanakuza na baadae kuuza / kuchinja..., wewe unachofanya ni kununua mifugo ambayo tayari imekuwa (hainyonyi) na kuipa chakula chenye lishe za kutosha ili wanenepe kwa kasi ya kutosha uweze kuwaweka sokoni.

Ingawa mimi sio mfugaji, nadhani dawa ni kununua mifugo kwa bei rahisi iwezekavyo, ikibidi kuifanyia castration na kuipa menu yenye virutubisho vya kutosha, na uwe na soko la kutosha ili wakifikia uzito tu unauza..., na unaendelea na game....
 
Kwa sasa kongwa wananunua kwa wakulima na kuchinja tu moja kwa moja
 
Nimetembea mashamba mengi ya serikali ila sijaona hii kitu. Huenda haiko profitable kwa mazingira ya hapa kwetu.
Shida Tanzania hatuna mazoea ya kununua vyakula kulingana na ubora(Quality). Sisi tunajali sana Quantity. Ukija na wazo la kuzalisha kwa ubora inakula kwako. Ndio maana super market ni chake sana. Watu wamezoea kununua vyakula kwenye masoko mjinga,ambako buku moja mtu anapata nyama ya kutosha.
 
Nikweli kabisa, hii system ili upate faida unatakiwa uwe na soko lako special, either supermaket au Hotel za kitaliii au ku export. Ila ukianza kushindana na wamasai lazma ule hasara tuuu.
 
Nikweli kabisa, hii system ili upate faida unatakiwa uwe na soko lako special, either supermaket au Hotel za kitaliii au ku export. Ila ukianza kushindana na wamasai lazma ule hasara tuuu.
Uko sahihi,wengi wameingia na wengi wametoka!
In short,unahitaji timings mbili. Wakati wa kununua ili unenepeshe,na wakati utakapouza baada ya kunenepesha.
Ukishajua hayo,kinachofuata uwe na elimu ya msingi katika unenepeshaji. Hii elimu kwa sasa inatolewa na Vyuo vya LITA,chini ya Wizara ya Mifugo na uvuvi.
Ni mafunzo ya muda mfupi,na gharama siyo kubwa.
Goggle Lita.ac.tz,utapata address yao then waulize.
 
Wanaendelea Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…