Ni wazi Hakimu Michael Mteite na Thomas Simba walitoa hukumu zenye utata dhidi ya Sugu na akina Mbowe

Mbona unawatisha Mahakimu, kwani kesi hizo ndo za kwanza kutenguliwa na Mahakama za juu? Ni jamii gani hiyo unayosema watakaa nayo vipi? Kwani hizo kesi zilikuwa na uhusiano na jamii au ni uendawazimu wa hao akina Sugu wakishavuta mibangi yao. Chadema hamna maana kabisa
 
Alipewa rushwa ya ujaji baada ya hukumu ile.Ndipo tuliposhuhudia wimbi la mahakimu wakishindana kuwafunga na kuwanyima Dhamana wapinzani Ili wapate teuzi
 
Mbona Hakimu Thomas Simba umri wa kustaafu ulitimia mwaka 2019!! Aliongezewa miaka 2 kama shukrani kwa kuishughulikia CDM.

Halafu aliahidiwa kupata UJAJI na Mwendazake bahati mbaya Magufuli ametema ndowano kabla hajmpa Ujaji aliomuahidi
Wote walipewa ujaji kama shukrani ya kuishughulikia chadema hata baada ya kustaafu.
 
Katiba mpya kwa ajili ya mahakama huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…