Ni wazi kuwa baadhi ya Wabunge wamekosa sera au waliingia Bungeni bila kujua wajibu wao

Ni wazi kuwa baadhi ya Wabunge wamekosa sera au waliingia Bungeni bila kujua wajibu wao

boniuso

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
786
Reaction score
1,043
Hilo nililolisema naamini kila mmoja wetu humu kama ni mfuatiliaji wa Bunge atakuwa ameliona

1. Hoja za wabunge juu ya kumuongezea rais muda wa uongozi.

Swali fikirishi hapa ni ‘Je, ni kweli hiki ndicho wananchi wa baadhi ya majimbo wanakitaka kutoka kwa wabunge wao?’ Yaani hawataki shule, barabara na maji ila wanataka tu Rais aongezewe muda?? Maana mbunge ni sauti ya wananchi. Au ni wabunge wanajikomba na kukosa chakuongea yaani hawana lamaana ila wamepata nafasi ya kuzungumza?

2. Sifa kwa rais zimekuwa nyingi mpaka zinaudhi.

Kila anayesimama awe Waziri, Mbunge ama Naibu Waziri ataanza na ahsante zilizopitiliza mpaka unaweza jiuliza "hizi sifa ni kweli au unafiki tu?”

3. Nimeumia sana na kauli ya Mbunge aliesema Bungeni ni kutamu na unaweza tamani hata kumwaga damu.

4. Hakuna maswali ya kama ya mabunge yaliyopita, hakuna mijadala migumu, wanaulizana maswali tu ili kutimiza wajibu.

5. Ahsante sana kwa Nape kwa swali na maoni juu ya wafanyabiashara na juu ya njia zinazotumika kukusanya kodi. Nimempa ahsante kwakuwa kajaribu kuhoji na kuchangia vile vitu jamii inataka kusikia.
 
Braza pesa ni mazingira, ndiomana hoja ya mwisho nimesema kabisa. Mazingira mazuri ya ukusanywaji kodi yatafanya tupate pesa." Kifupi nikwambie hivi sera na dira ya nchi ndivyo vitakuongoza wew kufanya unachotaka" .anyway kama wakuelewa umeelewa naamin
Tafuta hela wewe!
 
Sera na utafutaji pesa wapi na wapi? Karibu ununue Barakoa na Sanitizer
 
5. Ahsante sana kwa Nape kwa swali na maoni juu ya wafanyabiashara na juu ya njia zinazotumika kukusanya kodi. Nimempa ahsante kwakuwa kajaribu kuhoji na kuchangia vile vitu jamii inataka kusikia.
Tatizo mwisho alirudia matapishi yake kwa kuunga mkono hoja
 
Sera na utafutaji pesa wapi na wapi? Karibu ununue Barakoa na Sanitize
Ahsante sana, usisahau nyungu. Ila sera zikiwa bora za biashara hautaona kila kijana anaemaliza chuo anaweka status za kuuza nguo kweny status zake.
 
Ahsante sana, usisahau nyungu. Ila sera zikiwa bora za biashara hautaona kila kijana anaemaliza chuo anaweka status za kuuza nguo kweny status zake.
Sera peleka Ufipa. Hapa Ni 7 tena
 
Tatizo linajulikana na hakuna wa kulisema na kulishughulikia, tuvumilia ila giza nene mbele

Wanasema aongoze miaka milelee, wanadai ni mteule huyu katumwa kutuokoa.
 
Back
Top Bottom