Nakumbuka nikiwa zangu msasani beach tumelala kwenye bot bovu alikuja jamaa anakimbia usiku tukamuuliza vipi, akasema kuna maaskari wametimba maskani kukamata wahalifu, basi ilikuwa kama saa tano usiku tukampa hifadhi, ilipo fika kesho asubuhi tukakuta hayupo na kaondoka na viatu vyetu.
Way back 2017 nikiwa katika project za ujenzi.
Enzi hizo Jiwe yupo on pick ya kutumbua tumbua watu.
Nilikuwa mtaalamu sana wa kusuka na kutengeneza matenki ya maji. ([emoji16]Siyo haya ya simtank ni ya miradi ya maji)
Sasa akatokea jamaa mmoja hivi engineer (DWE) akawa analeta ujuaji mwingi mixer kujifanya kasoma sana akawa analeta mbwembwe za darasani. (Miradi mingi ya maji mafundi wa mitaani ndiyo wapo competition kuliko wasomi, Kampuni nyingi zinatumia mafundi kusuka na kutengeneza na ikiwezekana ushauri wa kitaalamu)
Kila nikumuelewesha anajifanya machinoo, muhuni nikakaa pembeni kuhepusha kuonekana bashite.
Lahaula zimebaki siku chache mradi ukamilishwe tanki likawa Linavuja na Maji yakawa hayana presha ya kupanda juu ya tank [emoji38].
DWE akanitafuta kusema anaomba msaada wangu na blaha blaha kibaoo,maana Kipindi hicho waziri alikuwa on fire kweli kutumbua tumbua.
Mwamba nikaamua kufoji na kufoji na kukubali kubebeshwa zigo lote.
[emoji16]Ajabu siku anakuja Eng Lwenge ndiyo alikuwa waziri wa maji wakati huo.
mwamba nikashangaa ana nisnitch kuwa kampuni YETU imeshindwa kutekeleza mradi na blaha blaha kibao.
Kilichotokea Serikali ikagoma kutulipa pesa zetu (Enzi hizo ulikuwa unajenga kwa pesa yako, mradi ukishakamilika ndiyo unalipwa chako).