Ni wiki tatu sasa msanii Harmonize hajatimiza ahadi ya gari ya 10M aliyomuahidi Shilole

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi.

Kwenye sherehe harusi ya Msanii wa muziki Shilole baadhi ya wasanii walitoa ahadi nyingi na wengi sana walitoa ahadi lakini kulingana na taarifa za kamati ya ufatiliaji wa ahadi zilizotolewa siku hiyo hadi sasa 99.9% ya ahadi zilizotolewa siku hiyo hazijatimizwa na hakuna dalili yeyote ya ahadi husika kutimizwa....
Kati ya watu walio toa ahadi kwa Shilole na Mmewe ni msanii mmakonde Harmonize na Mzungu wake wa Arusha ambao kwa pamoja waliahadi kumnunulia Shilole gari yenye thamani ya Million 10 wakishaichagua wawambie hata kama ni leo au kesho...baada ya ahadi ile ukumbi ulilipuka kwa vifijo na nderemo kutokana na ahadi ya uhakika na ya haraka ailiyotoa Konde Boy.....

Baada ya harusi kamati ilibidi kuanza kufatilia ahadi za watu walio toa lakini kamati iliona ianze na ahadi ya msanii Harmonize ambayo ilionesha ni ya haraka sana na alionesha anataka kuitimiza haraka sana..... baada ya kupata aina ya gari walio hitaji wahusika kamati walimpelekea ujumbe Harmonize lakini hadi sasa Harmonize amepiga kimya as if si yeye aliyetoa ahadi ile na wala hajibu sms za wana kamati wala hatoi ushirikianoe

Kwakuwa ahadi ni deni wana kamati wamejipanga kuonana na uongozi wa Harmonize ili wajue watatimiza vipi hiyo ahadi aliyotoa msanii wao.....

Wasalaam wana jamvi
 
Taarifa za mtaani zinasema pedeshee harmonize aka konde boy ameshanunua gari husika bado kulikabidhi tu.
 
Taarifa za mtaani zinasema pedeshee harmonize aka konde boy ameshanunua gari husika bado kulikabidhi tu.
mmmmh makubaliano yalikuwa ni shilole kuchagua gari na konde kutoa hela hahaha
 
Wanamuiga mlezi wao ama nin ahadi za kwenye mic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…