Niliambiwa mafua hayana dawa nimejaribu vumilia ila sasa ni wiki ya tatu nimeamua kumeza piriton doz ya 1mara2 kuna njia nyingine naweza fanya kwa sasa hali ya hewa pia ni barid nayo nadhani inachochea ila mbona mimi tu. Msaada plz
Niliambiwa mafua hayana dawa nimejaribu vumilia ila sasa ni wiki ya tatu nimeamua kumeza piriton doz ya 1mara2 kuna njia nyingine naweza fanya kwa sasa hali ya hewa pia ni barid nayo nadhani inachochea ila mbona mimi tu. Msaada plz
Mafua ni katika maradhi mabaya kwakweli kwani sehemu yenyewe ya pua ina mishikano na sehemu zote za uso, kwahivo husababisha maradhi zaidi ya mafua mfano husababishwa kuumwa na kichwa mara kwa mara, masikio hata na meno pia. Mafua hutokana na sababu nyingi tofauti nazo ni kama vumbi joto, na vitu vibaridi ambavyo hivi ndio huwa chanzo kwa mafua. Inshallah nitajaribu kuandika dawa moja lakini inafanya kazi kwa mara moja na ni dawa nzuri kabisa.
KITUNGUU SOMU:
Kitunguu Somu ni kinga ya maradhi mengi mno, na pia ni dawa ambayo ndani yake kuna vitu vinavyojulikana kwa "ALLICINE" NA "GARLICINE" ambavyo vina nguvu kubwa ya kupigana na wadudu.
Meza tembe (chembe) moja ya thaum kila baada ya chakula na pia unywe juice ya kitunguu Somu iliyochanganywa na maji ya ndimu na pia unaweza kujifukiza mvuke wa kitunguu somu.
Inshallah natumai dawa hii itakusaidia ila nakuomba kitu kimoja uwache kula vitu vibaridi sana na vitu vikali sana. Hata hivo nitachangia kidogo juu ya madhara ya Kitunggsomu, kitu chochote ambacho utatumia zaidi au utatumia bila mpango maalum basi lazima huleta madhara kwahivo kila kitu kitumiwe kwa kiwango fulani ili kujiepusha na madhara ya hicho kitu chenyewe.@G spanner.@Baba V