Ni wivu au kushindwa kujiamini?

bacha

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2010
Posts
4,282
Reaction score
797
Habari zenu wapendwa katika jina la bwana?
Nawapenda nyote, ila sijui kama nina wivu na nyie ama la!

Nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa na kutambua kuwa kuna sababu nyingi zinazoweza kumpelekea mtu kuwa na wivu, ingawa pia hali hiyo haikwepeki kwa vile iko kwenye mfumo wa kihisia zaidi za kibinadamu.
Wakati mwingine ni vigumu kuthibitisha hisia za wivu hali hiyo inapotokea.
Kuna aina nyingi za wivu lakini hapa nazungumzia wivu katika mahusiano ya kimapenzi, wivu huu umegharimu sana maisha ya wapendanao. Wengine kuuana, kutalikiana n.k. Isitoshe bado wengi wanasema kuwa mapenzi bila wivu hayanogi!!!!

Je,ni kwanini basi uwe na wivu kwa mpenzio?
Je, mahusiano ya kimapenzi bila wivu yanawezekana?
je, hali hii tunaweza kuita ni wivu au kutojiamini?
 
ukiwa na wivu mwenzangu ndio utamfaidi mpenzi wako lakini (usipitukie)maana huleta hisia yakuwa kweli fulani anipenda... kwanza....pili wivu unakufanya ujihisi uko peke yako kwake.
 
wivu ni muhimu sana.....!wivu huamsha hisia za mapenzi kwa yule umpendae...LAKINI SASA usiwe wivu wa kupitiliza
 
ukiwa na wivu mwenzangu ndio utamfaidi mpenzi wako lakini (usipitukie)maana huleta hisia yakuwa kweli fulani anipenda... kwanza....pili wivu unakufanya ujihisi uko peke yako kwake.

Nakuunga mkono. Hivi Nilham lile duka pale kariakoo lenye bango la avatar yako ile ya mwazo ni lako? Maana siku nilipokatisha na kuliona nilistuka!
 
Bila wivu atajuaje kama nampenda?
 
Wivu ni kero ndugu zangu.................................unapimwaje ili tuweze kujua kuwa wivu umepitiliza!!!
 
Wivu ni SUMU mbaya sana kwenye mapenzi wajameni...IT DEPENDS na jinsi mtu unavoweza kuuhandle

wengine unazidi hadi unakuwa GUBU kiabisa

Mi niulize tu katika muktadha huu, kwa nini nyumba ndogo 'zinauma' zaidi kuliko kubwa......hivi nao huo ni wivu ama GUBU.....

MJ1 hapa najua unaweza kuwa na 'a second thought'
 
hee subhallah hebu nieleze best ukiweza njoo pm hii si avatar ni picha yangu mwenyewe binafsi then sijawahi kuwa africa hata kimatembezi... ni kweli hayo usemayo au ni jokes habibty hebu nambie uzri...
Nakuunga mkono. Hivi Nilham lile duka pale kariakoo lenye bango la avatar yako ile ya mwazo ni lako? Maana siku nilipokatisha na kuliona nilistuka!
 

Aisee hommie, nakabiliwa na hako kaugonjwa asee.
 
Usipokua nao hatajua unampenda..itapunguza raha kwa umpendae maana wa we unakua kama huna hisia nae vile!Ukizidisha inakua kero kwasababu itaonyesha hujiamini wala humuamini!Ukiwa na wivu kiasi itampa yeye furaha ya moyo na wewe utakua unamjali na unamkubali sana bila kuonekana hujiamini!
 
wawa hivi...
kila saa simu u(uko wapi ee katavi??? hebu fanya urudi kazini si umetoka tangu saa 3.oo mpaka hii na nusu hujarudi )
akikamata cellphone yako mbio inbox..
ukiongozana nae akutizama machoni usije ukatiza mwanamke..
mkitizama tv usiweke picha yenye mwanamke mrembo ukamkodolea macho hakutalalika tena hapo...etc...
Wivu uliozidi unakuwaje!
 
sasa ka edit post yako hapo juu isomeke accordingly hahahaha....mjukuu wapi leo?

Mjukuu yupi? si unajua nina foleni ya jukuuz? afu hebu kaangalie jamaa wa kupakata bata kakugaragaza kule.......
 
huko ni kutokujiamini na wala hakuna kingine
 
Wivu ni muhimu
Wivu ni kero
Wivu ni sumu mbaya

Sio mimi but according to JF members
 

hauoni hapo kuwa tayari umeishaanza kuwa na wivu kwa katavi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…