MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Twende kazi.
Mustakabali mzima wa maisha ya mwanadamu ni kupambana na mazingira yanayomzunguka na mwisho kufa.
Ukiacha vitabu vya dini na ustahilishwaji kwa kutumia mema na mabaya ya nadharia ya dini za mapokeo na za kiasili, bado tunatafuta kujua ni nani amefanya matumizi sahihi ya akili zake akiwa duniani.
Ieleweke kwamba kila mwanadamu ni mshindi kwa namna yake kutokana na malengo aliyojiwekea. Wenye malengo madogo na kuyafikia wanashangilia ushindi kama vile wenye malengo makubwa na wakayafikia.
Kupata mali au kupata elimu kubwa siyo viashiria vya matumizi sahihi ya akili, ikiwa mali nyingi za huyo mtu na vyeti vingi vya huyo mtu haviwezi kumsaidia mtu kupambana na changamoto za kimaisha na kijamii.
Wapo matajiri wengi ambao wanachangamoto nyingi sana za kijamii (kesi mahakamani, kushindwa kuhimili familia, kutokukubalika na jamii na hata kukosa furaha) hali kadhalika wasomi wengi ambao wameshindwa kutafsiri vyetu kuwa pesa.
Kwa muktadha huo basi, ni yapi matumizi sahihi ya akili zetu hapa duniani?
Mlevi mmoja aliwahi niambia, kwa kua sote hakika tutakufa, na huko tuendako hakujulikani, basi yeye anatafuta hela na kuzichoma kibiriti zote (kula bata) kwa maana, ukiacha jeneza na jezi za simba (sanda), hakuna utakachoingia nacho kaburini.
Bado naendelea kuuliza, ni yapi matumizi sahihi ya akili zetu hapa duniani.