Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Camarades...., Kwa manufaa yangu na ya wengine yoyote aliyeshawahi kufanya hii biashara naomba dondoo za yafuatayo:-
Natanguliza Shukrani;
Majibu ya Mdau Kwa Manufaa ya Wengine...
- Bei ya kawaida ya kununua vinywaji Beer na ya kuuzia (ya chini kwenye bars/glossary) hence faida ya kwenye kila chupa.
- Je ni kawaida beer zote zina faida sawa au kuna brand ina faida zaidi ya nyingine
- Spirits Konyagi Grants et al na Wines Faida zake zipo vipi.
- Leseni ya Biashara kwa mwaka malipo yake
- Kama kuna vijikodi vilivyojificha
Natanguliza Shukrani;
Majibu ya Mdau Kwa Manufaa ya Wengine...
bei ya kununua creti ya bia inatofautiana kulingana na aina ya bia.mfano safari,kili,tusker,serengeti na castle light cret ni 32500 na wewe ukiuza utapata shilingi 40,000 kwa bei ya shilingi 2000@chupa na ndio bei iliyopendekezwa,faida kwa kila chupa ni 375/: kwa bia aina ya castle creti inauzwa 36000 na wewe ukiuza utapata 44000/kwa bei ya 2200@chupa ,faida yake ni 400@ chupa.kwa ujumla bia nyingi faida yake ina cheza kati ya 375-400.upande wa spirit ndiko kwenye faida sana ila utokaji wake c mkubwa sana kama bia.mfano konyagi kubwa inanunuliwa kati ya 6000 na kuuzwa 7500-8000 (faida ni kati ya 1500-2000)viroba vinanunuliwa 11000 na kuuzwa 18000 faida ni 7000,.kuhusu leseni inategemea na halmashauri uliyopo ila nyingi ni shilingi 10,000 kwa mwaka,kama ni grocery.Malipo mengine ni kodi ya mapato ambayo utakwenda ofisi ya Tra iliyopo karibu na wewe watakukadilia kulingana na mtaji wako wa biashara utakao anza nao,ukisema kiwango kikubwa nao watakukadilia hivyo hivyo.Nadhani utakuwa umepata picha halisi ya biashara hii kama utakuwa na swali lolote karibu