Ni Zipi Secret of the Trade Bar/Glossary ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Camarades...., Kwa manufaa yangu na ya wengine yoyote aliyeshawahi kufanya hii biashara naomba dondoo za yafuatayo:-
  • Bei ya kawaida ya kununua vinywaji Beer na ya kuuzia (ya chini kwenye bars/glossary) hence faida ya kwenye kila chupa.
  • Je ni kawaida beer zote zina faida sawa au kuna brand ina faida zaidi ya nyingine
  • Spirits Konyagi Grants et al na Wines Faida zake zipo vipi.
  • Leseni ya Biashara kwa mwaka malipo yake
  • Kama kuna vijikodi vilivyojificha

Natanguliza Shukrani;

Majibu ya Mdau Kwa Manufaa ya Wengine...

 
Wakuu yaani humu hakuna mwenye hii biashara au inakuwaje...

Anyway nimepeleleza mwenyewe kidogo kwa wadau nimesikia kwamba faida ni kati ya 200 mpaka 500 kwa chupa; lakini sana sana ni 200/= kwenye beers. Kwahio wadau wanasema nyama choma wa kwenye bar anaweza akawa anapata zaidi kuliko muuza vinywaji

Je ni ya kweli hayo?
 


Faida inaweza kuongezeka kutokana na eneo unalouzia. Wewe hujawahi kununua bia sh. 5000 kwa chupa wakati bia ile ile inazwa2500?

Tafuta eneo zuri. Vinywaji vinalipa asikwambe mtu. Ukimpata mtu mzuri wa jikoni ni vema zaidi.
 
Faida inaweza kuongezeka kutokana na eneo unalouzia. Wewe hujawahi kununua bia sh. 5000 kwa chupa wakati bia ile ile inazwa2500?

Tafuta eneo zuri. Vinywaji vinalipa asikwambe mtu. Ukimpata mtu mzuri wa jikoni ni vema zaidi.
Ndio maana nikasema pa kuanzia yaani ile lowest ya walala hoi..., sababu hapo unapochaji buku tano lazima pawe ni sehemu ya kiwango (yaani watu hawaji tu kupoza koo ni sehemu mandhari ni nzuri zaidi).., kwahio kwa kawaida bei ya mtaani faida ni 200/= mpaka 500/= ?

The reason nimeanzisha huu uzi kuna mtu nataka kumshauri ana sehemu nzuri anataka kufungua a small bar sasa ninamfanyia opportunity cost sababu nimeshamwambia akodishe jiko (kuondoa usumbufu na sio mtu wa kuweza ku-manage / uangalizi mzuri) ila sababu drinks ni rahisi kidogo kufuatilia ndio nataka nione kama its worth it asimamie yeye au na hili akodishe
 

bei ya kununua creti ya bia inatofautiana kulingana na aina ya bia.mfano safari,kili,tusker,serengeti na castle light cret ni 32500 na wewe ukiuza utapata shilingi 40,000 kwa bei ya shilingi 2000@chupa na ndio bei iliyopendekezwa,faida kwa kila chupa ni 375/: kwa bia aina ya castle creti inauzwa 36000 na wewe ukiuza utapata 44000/kwa bei ya 2200@chupa ,faida yake ni 400@ chupa.kwa ujumla bia nyingi faida yake ina cheza kati ya 375-400.upande wa spirit ndiko kwenye faida sana ila utokaji wake c mkubwa sana kama bia.mfano konyagi kubwa inanunuliwa kati ya 6000 na kuuzwa 7500-8000 (faida ni kati ya 1500-2000)viroba vinanunuliwa 11000 na kuuzwa 18000 faida ni 7000,.kuhusu leseni inategemea na halmashauri uliyopo ila nyingi ni shilingi 10,000 kwa mwaka,kama ni grocery.Malipo mengine ni kodi ya mapato ambayo utakwenda ofisi ya Tra iliyopo karibu na wewe watakukadilia kulingana na mtaji wako wa biashara utakao anza nao,ukisema kiwango kikubwa nao watakukadilia hivyo hivyo.Nadhani utakuwa umepata picha halisi ya biashara hii kama utakuwa na swali lolote karibu
 

Nadhani umemaliza kila kitu mdau; ngoja niweke na hii post yako hapo juu kama jibu kwa manufaa ya wengine asante sana mdau
 
Mkuu hapo kwenye Glossary ulikuwa umeniacha kidogo kumbe ni Grocery.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…