Ni zipi sifa na majukumu ya Mkuu wa Wilaya?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Wadau naomba kujua yafuatayo juu ya sifa za kuteuliwa Ukuu wa Wilaya na KAZI za MKUU wa WILAYA.

1. Elimu
2. Umri
3. Ujuzi
4. Itikadi
5. Uzoefu

Ili tusiwalaumu walioteuliwa kumbe wanasifa sahihi.

Pia je, kama sio Watumishi Taarifa zao zinapatikana Wapi maana hawana MAFAILI.

====

MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997).
(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971).
(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978).
(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1).
(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100).
(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18).
(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).
(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.
(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe.
(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi
(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.
(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.

From random individual somewhere in facebook
 
Msitegemee kigezo cha aina yeyote katika kazi yeyote kitafuatwa na serikali ya CCM, hawa watu wapo katika system ya kulindana kila mmoja ana mabaya na ndio yale yale yawale ukimwaga ugali namwaga mboga.

Watu hawafuati katiba ya Nchi watakuja kufuata vigezo. CCM haifai tena kuongoza nchi na ndio watakayoizamishaTanzania, wabaki kukata viuno kwenye majukwaa ndio ibada waliyonayo.
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya, msimamizi wa mapato na mpango mkakati wa wilaya, kuhakikisha jukumu la utawala linafanyika kiufanisi katika wilaya, mteule wa raisi( mwakilishi wa raisi) wilayani.nk

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Ni wahujumu uchumi tu hao. Serikali kila mwezi inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa umma, lakini usikute nusu ya hizo fedha hutumika kuwalipa mishahara watu wanaoteuliwa kwa ajili tu ya kuhakikisha ccm inabakia madarakani milele.
 
Wilaya ina mkuu DC, DAS, DED yaani matumizi ya hovyo kwa kuwapa watu mavyeo mengi ambayo yangeweza kufanywa na mtu mmoja
 
MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997).
(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971).
(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978).
(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1).
(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100).
(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18).
(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).
(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.
(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe.
(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi
(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.
(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.

From random individual somewhere in facebook
 
Kufungua makongamano ya Ukimwi , kuratibu mbio za mwenge , kuhamasisha usafi na ujenzi wa vyoo bora , pamoja na kuilinda ccm kwa udi na uvumba
 
Wadau naomba kujua yafuatayo juu ya sifa za kuteuliwa Ukuu wa Wilaya na KAZI za MKUU wa WILAYA.

1. Elimu
2. Umri
3. Ujuzi
4. Itikadi
5. Uzoefu

Ili tusiwalaumu walioteuliwa kumbe wanasifa sahihi.

Pia je, kama sio Watumishi Taarifa zao zinapatikana Wapi maana hawana MAFAILI.
Sifa kuu unatakiwa uwe kada mtiifu wa ccm! Masuala ya elimu, umri, ujuzi, na uzoefu kwa sasa siyo kipaumbele.

Yaani hata kichaa, jambazi, muuza madawa ya kulevya, mala.ya, nk. kwa sasa anaweza tu kuteuliwa kuwa DC, kwa sababu tu ni kada mtiifu wa ccm.
 
Wadau naomba kujua yafuatayo juu ya sifa za kuteuliwa Ukuu wa Wilaya na KAZI za MKUU wa WILAYA.

1. Elimu
2. Umri
3. Ujuzi
4. Itikadi
5. Uzoefu

Ili tusiwalaumu walioteuliwa kumbe wanasifa sahihi.

Pia je, kama sio Watumishi Taarifa zao zinapatikana Wapi maana hawana MAFAILI.

====
Nimeelewa
 
Naona mleta mada ulishapata muongozo...
Anaye tumia muda mwingi kwenye vyombo vya habari 'nyuma ya mikamera' wale ambao hawaonekani kwenye vyombo vya habari nadhani jibu nikwamba hawana uwezo wa kuongoza ndicho nilicho jifunza
 
MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997).
(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971).
(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978).
(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1).
(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100).
(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18).
(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).
(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.
(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe.
(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi
(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.
(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.

From random individual somewhere in facebook
(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.
Hili jukumu ndilo linatumika vibaya mara nyingi hutekeleza majukumu kinyume na sheria.
 
KKK.( Kusoma, kuhesabu na kuandika)
Uwe kada wa CCM
Ujue kutukana wapinzani hasa Chadema
 
Back
Top Bottom