Ni Zipi Tofauti za Madaraka na Mamlaka Kati ya Meya, Mkuu wa Wilaya na Mbunge?

Ni Zipi Tofauti za Madaraka na Mamlaka Kati ya Meya, Mkuu wa Wilaya na Mbunge?

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
774
Reaction score
1,464
Wakuu - Heshima Mbele


Naomba kuuliza ni zipi tofauti za madaraka na mamlaka kati ya Meya, Mkuu wa Wilaya na Mbunge. Na mipaka yao ni ipi. Pia kati yao ni nani anaongoza vitengo na taasisi gani? Mfano Mzuri ni Meya wa Ilala vs. Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mbunge wa Ilala (in 2012 ni Jerry Slaa vs Raymond Mushi vs Hassan Zungu)


NB: Kuna tofauti kubwa kati ya madaraka na mamlaka (responsibilities/duties vs. power)
 
Mayor is the highest-ranking officer in the municipal government of a town or a large urban city.In many municipal systems the mayor serves as chief executive officer and/or ceremonial official of many types of municipalities. Worldwide, there is a wide variance in local laws and customs regarding the powers and responsibilities of a mayor, as well as the means by which a mayor is elected or otherwise mandated


Head of the District
A
District Collector is the chief administrative and revenue officer of an Indian district. The Collector is also referred to as the District Magistrate, Deputy Commissioner and, in some districts, as Deputy Development Commissione

MP.

A Member of Parliament is a representative of the voters to a parliament. In many countries with bicameral parliaments, the term applies specifically to members of the lower house, as upper houses often have a different title, such as senate, and thus also have different titles for its members, such as "senators".

Members of parliament tend to form parliamentary groups (also called parliamentary parties) with members of the same political party. In everyday use, the term Member of Parliament is almost always shortened to the initialism "MP", and this is also common in the media.

Kuna Tofauti kubwa kati ya Meya mji au jiji,Mkuu wa wilaya na mbunge, kila mtu ana cheo chake na kazi yake. ila kati ya hao wote 3 Mkuu wao ni huyo Meya wa Mji anaye fuatia atakuwa ni mkuu wa wilaya kisha ndio aje huyo Mbunge wa wilaya. na kila mtu ana madaraka yake na kazi yake muhimu ndani ya Serikali.
 
Nashukuru

kwahiyo Meya ni Mkuu wa Halmashauri ya Mji. Na ndio msimamizi wa vitengo na taasisi zote zilizoko chini ya halmashauri

Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa Serikali Katika Level ya Wilaya. Ni Mwakilishi wa Rais na Mkuu wa Mkoa huko wilayani. Na mkuu wa vitengo na taasisi zote zilizoko chini ya serikali kuu

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika jimbo. kazi yake nikuwawakilisha na kuwasemea wananchi.

Hapa Tanzania hivi vyeo vinachanganya na kuingiliana sana na mameya, wakuu wa wilaya na wabunge wengi hawaelewi madaraka na mamlaka yao na mipaka ya madaraka yao.
 
Mkuu Ngwanakilala hivi vyeo vinafaa viangaliwe upya wakati wa kuandika katiba mpya.Ni vyema wakuu wa wilaya wakafutwa kabisa hawana kazi za kufanya sana sana wanatuongezea mzigo sisi walipa kodi.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kwetu Tanzania hivyo vyeo vyote vimekaa kisiasa kuliko kiutendaji na kuwatumikia watanzania. Meya anatakiwa achaguliwe na wananchi wa mkoa husika kila chama kitoe mgombea wake katika nafasi ya Meya pamoja na Naibu Meya.

Mbunge yeye anatakiwa kusimamia eneo lake la jimbo kama mbunge. Pamoja na kuwa muwakilishi bungeni.

Mkuu wa Wilaya cheo chake kimekaa kisiasa zaidi kazi ya Mkuu wa Wilaya inatakiwa ifanywe na mkurugenzi wa wa usalama wa wilaya.
 
Mkuu Ngwanakilala hivi vyeo vinafaa viangaliwe upya wakati wa kuandika katiba mpya.Ni vyema wakuu wa wilaya wakafutwa kabisa hawana kazi za kufanya sana sana wanatuongezea mzigo sisi walipa kodi.


Nakubaliana na wewe na ndio maana nikauliza. Yani hivi vyeo ni vurugu na mkanganyiko. Kuna wakuu wa wilaya wana elimu ya darasa la saba na wengine wana PhD. Kuna wakuu wa wilaya ni makanali wa jeshi na wengine ni makaptain. Kuanzia uteuzi wao, madaraka, mamlaka mpaka utendaji wao ni mkanganyiko mtupu. Hiki cheo no kichaka na CCM kulipana fadhila. Katiba lazima iangalie upya hiki cheo.

Umeya wenyewe sikujua kuwa una madaraka na mamlaka makubwa mpaka yule Meya Jerry Slaa alipoanza kufanya kazi zake ndio nikashutuka na kuanza kujiuliza sasa mameya wengine wanafanya nini?

Ubunge nao - we all know katiba inabidi iangalie uwezekano wa kufuta viti maalumu. Uongozi dhaifu huzaa serikali dhaifu
 
Tatizo kwetu Tanzania hivyo vyeo vyote vimekaa kisiasa kuliko kiutendaji na kuwatumikia watanzania. Meya anatakiwa achaguliwe na wananchi wa mkoa husika kila chama kitoe mgombea wake katika nafasi ya Meya pamoja na Naibu Meya.

Mbunge yeye anatakiwa kusimamia eneo lake la jimbo kama mbunge. Pamoja na kuwa muwakilishi bungeni.

Mkuu wa Wilaya cheo chake kimekaa kisiasa zaidi kazi ya Mkuu wa Wilaya inatakiwa ifanywe na mkurugenzi wa wa usalama wa wilaya.


True indeed. Sielewi kwanini serikali inapoteza hela kulipa wakuu wa wilaya ambao technically ni matarishi tu wa serikali kuu.
 
Back
Top Bottom