Ngwanakilala
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 774
- 1,464
Mkuu Ngwanakilala hivi vyeo vinafaa viangaliwe upya wakati wa kuandika katiba mpya.Ni vyema wakuu wa wilaya wakafutwa kabisa hawana kazi za kufanya sana sana wanatuongezea mzigo sisi walipa kodi.
Tatizo kwetu Tanzania hivyo vyeo vyote vimekaa kisiasa kuliko kiutendaji na kuwatumikia watanzania. Meya anatakiwa achaguliwe na wananchi wa mkoa husika kila chama kitoe mgombea wake katika nafasi ya Meya pamoja na Naibu Meya.
Mbunge yeye anatakiwa kusimamia eneo lake la jimbo kama mbunge. Pamoja na kuwa muwakilishi bungeni.
Mkuu wa Wilaya cheo chake kimekaa kisiasa zaidi kazi ya Mkuu wa Wilaya inatakiwa ifanywe na mkurugenzi wa wa usalama wa wilaya.