HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Songíto;3456491 said:Aisiiiii!! hili ni la kiundani zaidi... ningeweza kukuuliza maswali lakini tayari yamejibiwa kwenye ujumbe wako maana unasema mwenendo wako hauna mashaka... Tu je unahakika kuwa vile unavyoona kuwa mwenendo wako hauna mashaka ndivyo mwenzio anavyoona pia? isije kuwa wewe ndo unaona halafu yeye anakutilia shaka!!
Kifupi ni kwamba lipo jambo, mimi na wewe hatujui.. hebu jitoe siku moja, mvizie wife akiwa katika mood nzuri, msuprise na kazawadi kokote ka kimahaba, na akiwa katika furaha wakati anapokea, mwombe utoke nae out na umwambie kuwa una mazungumzo nae!! mpeleke mahali penye hadhi kubwa kidogo, namanisha pazuri na patulivu, iwe hotelini au ufukweni ambapo mtapata chakula na kuongea mengi, mkumbushe jinsi mlivyokuwa mmeanza mahusiano na vitu vingine ambavyo vitamfanya afurahi na kutabasamu
mkiwa katika maongezi mwambie kwa upole na unyenyekevu kuwa unaona tatizo katika ndoa kwa mida hii, ila usimlaumu yeye, useme tu unajisikia vibaya na ungependa mzungumze ili mpate suluhisho la pamoja nae, naamini atafunguka na utajua nini kinamtatiza.
Ukiona zaidi ya hapo hataki basi ujue ana gubu tu na si rahisi kumbadili
Ungemwambia kuwa: "Mwanamke anapaswa kufanya anachoambiwa na mke wake" maana hicho ndicho unaamini.
Sasa sisi tushauri nini hapo!
Baada ya kujaribu ushauri mwingi ulopewa na wachangiaji mbalimbali, hebu kaa chini ufikirie hayamaswali yafuatayo: Wanawake wengi wanapenda kuwa na security ya maisha. Je mnaishi mjini? Je mtoa thread anaishi na wazxazi wake au hawa wazazi wako mbali na mji mnaoishi? Kama wazazi wa mwanaume wanaishi mbali na mji mnaoishi, je umeshapata kumpeleka mkeo huko kuwaona wazazi? (wakwe wa mkeo) Je mahusiano yako(mleta thread) na wazazi wa mkeo yakoje? Kama mahusiano na wakwe(pande zotembili) hayako sawa, linawafanya wanawake wengi kukosa amani.Wasalaam,
Mimi ni kijana mwenye familia ya mke mmoja na mtoto. Sijwahi kuwa na ugomvi na mke wangu isipokuwa tangu mwezi uliopita, amekuwa yuko kimya sana (amepoa sana) na hachangamki hata ukimsemesha au kumtania. Jibu lake limekuwa "Niache bwana, nina mawazo yangu!". Nimetafakari mwenendo wangu kwa muda mrefu hauna mashaka yeyote.
Najiuliza tatizo ni nini maana hali yake hii inanisikitisha na kuniyumbisha kisaikolijia. Naomba mawazo na ushauri wenu wa dhati ndugu zangu kuhusu nini cha kufanya ili nijue tatizo lake. Wenzangu wake zenu wamewahi kuwajibu hivyo? Mlifanyaje?
****** Imetumwa na Johnson, Mara Musoma ********