Real experience kwenye Toyota IST ncp61 (cc 1490).
Fuel consumption iko poa sanaaaa, inanusa!
Long safari, kinafaa ikiwa wewe ni wale wenzagu namimi wa 'ilimradi kufika safari' bila kujali stability & comfortability. Kwa long safari usivuke speed 130! ukivuka hapo kanakuwa kepesi kama sufi, katapeperushwa na semi tutakuokota vichakani. Comfortability ni zeroooo, long trip utafika kiuno na mgongo viko hoi taabani.
So to summarize, baby walker IST haifai kama ni mtu wa safari ndefu mara kwa mara, katakuua mgongo na kiuno. Na pia hakafai kabisa kama unapenda speeding, stability ni sifuri.
Lakini kama ni mtu wa town trips na mishe za hapa na pale, kanafaa. Cheap and affordable maintenance.
Nadhani Subaru inaizidi IST kwa kila kigezo. Subaru yaweza kuwa ni gari. Ila IST ni chombo cha usafiri kukusogeza hapa na pale tu.
Mie saahivi nawaza baby walkers za mjerumani. Watemi wa mjini wana kamsemo: "ukitaka safety, speed, na comfortability, nenda kwa mjerumani".