Nichague ipi kati ya IST na Subaru Impreza

Wakuchanja

Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
82
Reaction score
54
Wakuu kwema

Nataka kuvuta mchuma kati ya Subaru Impreza na ist naombeni ushauli wenu juu ya hayo magari ili nifanye chaguzi sahihi.


Subaru Impreza


Toyota IST
 
Me nakushauri chukua hizi ist new model ni gari ziko pw sanaa kuanzia fuel consumption na comfortablity wakati unachanja mbuga...hizi Subaru nazo siko vizur ila cjabahatika kuitumia.

Kila la kheri mkuu
 
Wakuu kwema

Nataka kuvuta mchuma kati ya Subaru Impreza na ist naombeni ushauli wenu juu ya hayo magari ili nifanye chaguzi sahihi

Kwa umadhubuti wa jumla, stability, na overall safety chukua Subaru Impreza ila kama priority ni gharama nafuu za kutunza na kuliendesha gari basi chukua IST.
Angalizo tu: Gari yoyote inahitaji matunzo na service za uhakika ili uifaidi kwa muda mrefu.
 
Wakuu kwema

Nataka kuvuta mchuma kati ya Subaru Impreza na ist naombeni ushauli wenu juu ya hayo magari ili nifanye chaguzi sahihi
Subaru impreza ni gari nzuri, iko fasta hasa katika long safari. Pia ni sport car, na inatulia barabarani. Shida ni pale utaitaji spare parts, kidogo bei imechangamka na sio nyingi kivile. Ila utazipata.

IST nayo ni gari nzuri sana. Fuel consumption iko poa sana hasa zike za 1290. Ingine zake ni nzuri sana hata kwa safari ndefu. Ndio maana IST nyingi ni urber hapa bongo. Hazina shida na mafuta. Hata uweke ya kidumu porini chenyewe kina kupa support. Spare zake ni nyingi mno, kama maharage hapa bongo. Hata uwe na buku jero utakula tu.

Kama alivyosema mi_mdau gari ni matunzo. Zingatia service time kila mara. Usiwe mtu wa mashindano barabarani.

Drive safe mkuu,
 
Subaru impreza ni gari nzuri, iko fasta hasa katika long safari. Pia ni sport car, na inatulia barabarani. Shida ni pale utaitaji spare parts, kidogo bei imechangamka na sio nyingi kivile. Ila utazipata...
Subaru Impreza naipenda ila naona kama Ground Clearance yake iko chini sana, kwa hizi barabara zetu si shida sana?
 
Subaru Impreza naipenda ila naona kama Ground Clearance yake iko chini sana, kwa hizi barabara zetu si shida sana?

Yeah ground clearance iko chini na bumper zake za mbele ni ndefu (hazina approach angle nzuri). Kwa hiyo kwa hizi njia zetu lazima ukubali yafuatayo:

1. Kubali kuwa ni gari ya chini kama zilivyo BMW Sries 3, Benz, Crown etc. So kuwa makini.

2. Ufunge rim na tairi kubwa kidogo.

3. Ufunge coil ndefu au heavy duty (ila gari itakuwa na stiff ride).

4. Ufunge spacer (mi bunafsi huwa sipendi hii option ambayo ndo rahisi kuliko zote).
 
Hii gari ni nzuri ila ni changamoto sana. kwa njia zetu hizi
 
chukua IST gharama za utunzaji ztapngua na wese inanusa tu...ila kidizain hizi hatchback huwa sizielewi kwakwel zna shape mbaya.., kwann usi opt kwenye SEDAN ukachkuwa Allion...alaf upate black[emoji16][emoji16] yaan ni balaa wawez ksema boss nani huyu anapita, ukipita nalo mtaani.

Allion gari nzuri, spare zipo za kumwaga mana toyota, halafu ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana, mana inaenda 18 km per 1 lt....
halafu ina range ya cc 1490, itakuwa na nguvu kuliko IST mkuu..., chukua toyota Allion hutojuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subaru Impreza naipenda ila naona kama Ground Clearance yake iko chini sana, kwa hizi barabara zetu si shida sana?
Kama ipo chini si unainyanyua mjomba?
 
Kunyanyua siyo option nzuri sana, ni rahisi sana gari kupoteza stability na comfortability
Basi ni hivi mdau ni either ununue gari ilioinuka cross over au SUV au iliochini (saloon) hapo hauna option
 
Basi ni hivi mdau ni either ununue gari ilioinuka cross over au SUV au iliochini (saloon) hapo hauna option

Kama anaweza kuishi na hizi changamoto anunue tu, siyo kwamba atashindwa kutumia kabisa. Naona wengi tu hasa dar hapa wananunua tu magari ya chini kama crown na nyinginezo na wako comfortable tu. Kuna gari nyingi tu ziko chini kuliko Impreza. Binafsi zinanipa shida kiasi na ilichangia mi kuiuza
 
Dar njia nyingi ni za Lami, gari haichoki haraka uvunguni wala kwenye bumper lenyewe, labda uwe rough uligonge gonge hovyo.
 
Real experience kwenye Toyota IST ncp61 (cc 1490).

Fuel consumption iko poa sanaaaa, inanusa!

Long safari, kinafaa ikiwa wewe ni wale wenzagu namimi wa 'ilimradi kufika safari' bila kujali stability & comfortability. Kwa long safari usivuke speed 130! ukivuka hapo kanakuwa kepesi kama sufi, katapeperushwa na semi tutakuokota vichakani. Comfortability ni zeroooo, long trip utafika kiuno na mgongo viko hoi taabani.

So to summarize, baby walker IST haifai kama ni mtu wa safari ndefu mara kwa mara, katakuua mgongo na kiuno. Na pia hakafai kabisa kama unapenda speeding, stability ni sifuri.

Lakini kama ni mtu wa town trips na mishe za hapa na pale, kanafaa. Cheap and affordable maintenance.

Nadhani Subaru inaizidi IST kwa kila kigezo. Subaru yaweza kuwa ni gari. Ila IST ni chombo cha usafiri kukusogeza hapa na pale tu.

Mie saahivi nawaza baby walkers za mjerumani. Watemi wa mjini wana kamsemo: "ukitaka safety, speed, na comfortability, nenda kwa mjerumani".
 
Nadhani kwa ujumla Subaru ipo vizuri zaidi ya ist

Lakini sasa inapokuja kibongo bongo ist itakufaa zaidi kwa sababu spea zake bei nafuu na nyingi mitaani kuliko za subaru
Hata mafundi wa Toyota bei zao sio mbaya kama ukipeleka brand zingine za magari kama subaru. Kwenye ulaji mafuta bado ist atakua anafanya vizuri zaidi ya subaru.

Kwenye barabara zetu subaru yupo chini sana kulinganisha na ist

Ila sasa ukiingia baa ukapiga vyombo vya kutosha hukawii kukutwa unahangaika kufungua gari ya watu kwa jinsi zilivyojaa na kufanana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…