Nichague ipi kati ya Nissan Extrail na Toyota Rush?

grandMullah23m

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2017
Posts
245
Reaction score
331
Wanajamvi,

Naomba kufahamu zaidi kati ya Nissan X-Trail na Toyota Rush Kwa msela kama Mimi ninayeanza maisha ni ipi inafaa zaidi kimatumizi ya kila siku, usalama, uwezo wa kupita na uendeshaji kwa baadhi ya maeneo ya hapa Dar na hata (mikoani), ufanisi wa mafuta, huduma na ufikiaji wa vipuri, gharama za umiliki.

Pia nikipata uzoefu na mapendekezo kutoka kwa wamiliki wengine itapendeza zaidi ili niweze kufanya uchaguzi unaofaa kulingana na mahitaji yangu na mazingira niliyopo.

NB: Nimepanga kuishi kibajet Kwa kuweka lengo la kufikia hapo bila kukopa benk[emoji848]

Yawezkana naota ndugu zangu, tutoane to ngo kidogo
 
Iwe unaota au unamaanisha, running cost za x-trail ni kubwa kuliko rush, lakini tukiongelea kimuonekano, x-trail iko vizuri. X-trail ina baby face (whether new model or old) wakati Rush ina elder face.
 
Rush ya mwaka gani na
X-trail ya mwaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…