Hello Ndg. Udochi
Bila shaka utakuwa unaendelea vizuri na shamrashamra za sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Mimi ni dalali wa magari na vilevile ni miongoni mwa wadau wa jukwaa la JF Garage linalohusu maswala ya vyombo vya moto. Ningependa kuchukua fursa hii kukujibu kupitia uzi wako uliokuwa ukihitaji ushauri wa aina gani ya gari ununue kulingana na bajeti yako ya TSh 10M za kitanzania. Kwanza kabisa nikupongeze kwa hatua nzuri uliyochukua ya kuja jukwaani kuomba ushauri kabla ya kufanya maamuzi ya kununua chombo cha moto.
Hakika kwa swali lako unaonekana umekwiva/komaa katika masuala ya ujasiriamali ambayo yanahitaji uvumilivu, subira na ushauri kutoka kwa wajuvi wa kada mbalimbali. Basi bila kupoteza muda ningependa niende moja kwa moja katika lengo hasa la kukufuata huku faraga. Kwanza kabisa unapotaka kununua gari ni vizuri ukaangalia ni aina gani ya matumizi unayotaka kutumia katika chombo husika. Nitegee sikio kwa makini kabisa, hivyo basi lazima utambue kwamba huwezi ukawa mkulima na kazi zako zinategemea kwenda shambani ukanunua gari ambayo sio madhubuti, au ukawa ni mkandarasi ukanunua chombo cha usafiri ambacho hakiendani na matumizi ya kazi zako za mara kwa mara hapo itakuwa ni sawa na kuharibu pesa.
Hivyo basi katika kulitambua hilo gari itakayokufaa kwa matumizi ya kawaida ya mizunguko yako mjini na kubebea bidhaa za dukani kwako mara moja moja ni zile zenye uwezo wa kula mafuta kwa kiasi kidogo, spare zake zinazopatikana kwa urahisi na bei nafuu, na zile zenye uimara wa engine, gearbox na muundo(Body), ili kuweza kukurahisishia katika ku-maintain chombo chako kwa gharama ndogo na kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Gari zenye ni kama vile ifuatavyo ;Vitz, IST, Porte, Funcargo, Passo, Sienta, Wish, Runex, Allex, Rumion, Platz, BB, Corolla X, Premio New & Old, Carina T.I Na S.I(Hizi zote zinatengenezwa na kampuni moja kubwa kutoka Japan inayoitwa TOYOTA yenye mtaji mkubwa kushinda kampuni yeyote Duniani wa takribani dolla Bilioni 200 hadi hivi sasa. Magari yao mengi wanayauza Afrika kutokana na kuhimili ukame na joto sambamba na spare parts zake kupatikana kwa urahisi na kuingiliana. Kwa mfano IST na Porte zinaingiliana kuanzia Engine, gearbox, hadi kwenye miguu(Shock-Up, Wishbon, Ball Joints n.k. na Hiyo ndio sababu hasa kukupendekezea gari zote za kampuni moja.
Kwa offer yako tunauwezo wa kupata gari mpya kutoka Japan na nikakufanyia usajili wa jina lako ukawa ndio mmiliki wa kwanza hapa Tanzania, au kama utahitaji ya bei ya juu kidogo kama vile Premio, Allex, au Allex tunaweza kupata ambayo haijatembea masafa marefu zaidi na ikakufaa kwa matumizi yako bila kuhitaji kushinda garage. Kwa hayo machache ningependa niishie tamati hapo.
Kama utakuwa na swali au chochote cha kuuliza tuwasiliane kupitia simu namba : +255 747 999 927 au kwa barua pepe
darautobroker@gmail.com. Tumejidhatiti kukuhudumia vyema na kwa weledi zaidi. Our Motto : Committed To Excellence