Nichukue gari ipi?

Nichukue gari ipi?

mgulu

Member
Joined
Feb 14, 2015
Posts
74
Reaction score
34
Wakuu naombeni mnisaidie nataka kununua gari, sina uzoefu wa aina yoyote wa magari.
Ushauri wenu muhimu sana.

1588717607.jpeg
rockcity%20cars%20used_73420177_162182624847679_4812119866917008353_n.jpeg
rockcity%20cars%20used_75214729_653049408553129_3950424101213915627_n.jpeg
 
Chukua ambalo moyo wako umelidondokea!!
 
Zote zaonekana ni gari zilizotumika hivyo tazama kiasi cha miles/ kilometer zilizotembea.

Zingatia matumizi ya mafuta, ni wazi hapo Brevis inatumia mafuta zaidi, then Voltz na mwisho Passo.

Je unaishi maeneo gani, hali ya barabara ikoje? Kama unaishi madongo kuinama ina maana walau Voltz itakufaa.

Je, una familia au lah. Kama jibu ni ndio basi Passo haikufai.

Zaidi tafuta fundi mzuri akusaidie kufanya ukaguzi wa kimakenika.
 
Ukiona mtu anatafuta gari mkononi kwa mtu basi pesa yake ni ya kuunga unga sasa ngoja nikushauri ili usijekwama hata kulipa ada ya watoto wako wawili!! ni hivi..Achana nazo gari zote hizo pichani tafuta IST ni ngumu na economy na inatengenezeka kirahisi.. au tafuta premeo au carina ni gari common na mafundi wengi wanazijua vizuri hutopata shida ya servicing.. tena hiiyo brevis ndio jini mnyonya damu usijaribu kabisaa
 
100%
 
Mtu akikuuliza kati ya ndizi, chungwa na nanasi ninunue tunda lipi?

Je, jibu lako litakuwa "nunua muhogo"?

Mnaosema Voltz ni gari nzuri mnatumia vigezo gani?!?! Maana Toyota walishaacha kuyatengeneza mwanzoni mwa miaka ya 2000!!!

Anyway, according to Kidukulilo hayo sio magari, ni takataka flani hivi
 
Mnaosema Voltz ni gari nzuri mnatumia vigezo gani?!?! Maana Toyota walishaacha kuyatengeneza mwanzoni mwa miaka ya 2000!!!

Anyway, according to Kidukulilo hayo sio magari, ni takataka flani hivi

Cha ajabu huyo kiduku alikua anaulizia mafundi huko Tabata gx 110 yake miguu ya mbele inagonga.

Sasa sijui hio gx110 yake ni usafiri au gari?
 
kama hujui gari gani ya kuchukua kati ya hizo

mimi nakushauri chukua ki PASSO chako tulia jifiche ndani

ukishakua na akili ya kuchagua magari next time Sitoona PASSO kwenye list yako.
 
Mkuu kama ni gari yako ya kwanza chukua passo ila hakikisha ni pistoni nne haya ya pistoni tatu mimba sana. Iyo passo kwa kuwa ni gari ya kwanza uta enjoy kwenye ishu ya mafuta
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada....wewe ni KE au ni ME
Mkuu kama ni gari yako ya kwanza chukua passo ila hakikisha ni pistoni nne haya ya pistoni tatu mimba sana. Iyo passo kwa kuwa ni gari ya kwanza uta enjoy kwenye ishu ya mafuta
 
Back
Top Bottom