Wakuu, Town Ace na Lite Ace ni gari zinazoshare platform (rebadged), almost "kila kitu" vinafanana sema tu Lite ni kwaajili ya Lite duties na Town ni kwaajili ya Urban/town duties.
Sasa ikija issue ya kuchukua gari ipi, hapo kuna factors nyingi za kuangalia, mfano: matumizi, inafanya kazi wapi, na condition ya gari.
Izo mbili naona Ace ni ya muda sana 1995 wakati Lite ni 2002.
Kwakua umetupatia features mbili tu (mwaka na mafuta), mimi pia ningeenda na Ace kwasababu ya duties zake na Diesel.
Tungepata features zingine tungejua engine capacity, hp, millage etc.
Hiyo uliyotuwekea ni Town Ace M series 3rd generation (1986-2007). Zipo za Diesel na Petroleum.
Za Diesel ni cc 1900, 2000 na 2200 sijui yako hapo ngapi?
Ila ni nzuri, ina hadi Van zake kwahiyo usiogope mambo ya spare na Toyota hawanaga show mbovu.