Nichukue ipi kati ya IST na Corolla Runn X?

Allex na runx si ndugu tuu, bali ni kitu kile kile kimoja. Yaani ni gari ile ile tuu, majina yalitofautishwa kwa sababu ya masoko

Ni sawa na wewe uwe na jina la nyumbani na jina la shule
Kama Abdallah kumuita Dulla
 
Habari chief!

Spacio New Model ya mwaka gani ambayo iko vema kwa Cc 1490?
 
Mi binafsi nimeendesha zote Allex na Ist na sasa hivi natumia Allex, Allex zipo stable sana barabarani compared na Ist. Nilifanya test moja nilikuwa mwenyew kwenye gari kwa kuanza na Allex nilishusha vioo then nikatembea hadi 130 kupima stability ya gari. Allex ilikuwa imetulia sana ila kwa IST inanesa sana na nilifanya hivyo kwa Allion pia yote yakawa yale yale so nika conclude kuwa Allex ipo stable sana (na hapo nilikuwa mwenyew ndani ya gari)
 
Kuhusu kugusa chini nilichokifanya kwenye gari yangu niliinyanyua kidogo kwa nchi moja, pia tyre nikabadili kutoka 180 kwenda 195 na rim size nikachange kutoka 14 kwenda 15 basi gari yangu ipo juu kinyama kiasi kwamba sigusi popote pale
 
kama ana umbo kama la Piere Likwid au Dora na kama kweli hatobeba abiria hata iwe baba/mama/mke/mume/mtoto n.k basi achukue IST ila kama ana umbo la kawaida na kuwa ipo siku atabeba mtu mwingine basi aachane na IST
ina maana ist ina nafasi ya mtu mmoja tu?dereva tu.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…