Habari za asubuhi Wanajamvi leo Nina jambo na mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa kuweka mkazo mkubwa kwenye mgawanyo wa majukumu kwamba kama una changamoto kuhusu kitambulisho cha taifa unatakiwa uende kwenye mkoa, wilaya au kata uliojiandikisha hili ni zuri lakini kwa upande mwengine linachelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwani wapo wananchi wengine waliojiandikisha sehemu ambazo sio makazi Yao mfano waliopo kwenye makambi ya majeshi, wanafunzi mashuleni na vyuoni hivyo unakuta pindi vitambulisho vikitoka hawawezi kupata urahisi wa kuvipata kutokana na changamoto za umbali pia hata ikitokea taarifa zao za kwenye kitambulisho cha taifa zimekosewa hawawezi kubadilisha mpaka wafike kwenye ofisi walizijiandikisha hivyo kuwakosesha kupata vitambulisho vyao na kufanya markebisho ya taarifa zilizokosewa.
Baadhi ya wadau wanasema wamejiandikisha toka mwaka 2018 kwenye mikoa mbalimbali walipokuwa mashuleni na kwenye makambi ya jkt lakini Hadi leo hawatapata vitambulisho vya taifa wakifuatilia makao makuu wanaambiwa waende wakachukue walipojiandikisha hivyo kushindwa kupata haki yao ya kupata vitambulisho vya taifa
Pia wapo baadhi ya wadau ambao taarifa zao zilikosewa kipindi wanaandikishwa wameshindwa kwa madai waende walipojiandikisha
Baadhi ya wadau wanahoji ikiwa tuko kwenye kipindi cha maendeleo mkubwa ya sayansi na teknolojia ya habari ni kwann mamlaka ya vitambulisho vya taifa inashindwa kufanya huduma zote kupitia makao makuu kuliko kuweka mlolongo wa urasimu unaokwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi
Mdau mwengine akatolea mfano ikiwa mtumiaji wa mtandao wa simu aliyejisajili mkoani anaweza kuhudumiwa makao makuu ya mtandao husika inashindikana vipi kwa NIDA kufanya huduma zote makao makuu na kuwapunguzia wananchi gharama mbalimbali na vikwazo vinavyowakosesha kupata vitambulisho vya taifa
Nawasilisha.
Mwananchi wa kawaida.