NIDA Kagera hasa Wilaya ya Missenyi ni Mateso

NIDA Kagera hasa Wilaya ya Missenyi ni Mateso

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Habari wadau,
Heri ya mwaka Mpya 2020. Kuna haja ya kufuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye ofisi za NIDA mkoani Kagera hasa Wilaya ya Missenyi maana taarifa za mtu kupatikana pale ni jambo gumu.

Kama rushwa inahitajika basi waseme bei. Si kweli kwamba wakazi wa Wilaya ile wote sio Watanzania. Binafsi nimeenda nikauliza vipi mbona taarifa zangu hazionekani nikaishia kupewa namba ya simu kuwa niulize baada ya siku chache. Hiyo namba haipatikani kabisa so nilipunguzwa kiaina.

Hizo siku 20 hazitoshi, kama ni kutangaziwa kuwa sie sio Watanzania watu wa maeneo yale tuambiwe japo kadi za mpiga kura tunazo hizo hazina shida. Kwa presha hii na muda huu ni kutengenezeana mazingira ya kupeana rushwa tena kwa lazima.

Visingizio vingi mtu unaenda zaidi ya mara tatu unaambiwa hawawezi kuangalia taarifa zako maana wako offline. Sijui Offline kivipi. Kwa kifupi tumechoka. Basi fungeni line. Tunatoa hela zetu zote kwenye simu, kodi haitalipwa na makampuni yatapata hasara. Tutaanza kupigia simu vibandani kama zamani. Hali hii imesababisha kaya yenye watu zaidi ya watano, mtu mmoja kusajiri line zote za wanafamilia ili zisifungwe. Mtu atafanya uhalifu na mnakuja kukamata mtu asiyehusika. Inapofikia hatua unataka kumnyima mtu huduma kwa wewe kushindwa kutimiza wajibu wako ni uonevu wa hali ya juu.
 
Wananchi wanaoishi mipakani wilaya ya Missenyi watendewe na wahudumiwe sawasawa kama watanzania wengine.Wasinyanganywe mashamba na mifugo yao kwa visingiziyo kuwa mpakani mwa Uganda na Rwanda.Wananchi wa mipakani wanajuwana ni yupi ni raia au sio raia hivyo wapewe haki zao bila ya ubaguzi
 
Mbona matatizo kama hayo hayapo Sirari Tarime,Rorya, Namanga, Tunduma na kwingineko badala yake iwe Mkoa wa Kagera tu? Pana tatizo la ukimbizi hapo
 
Back
Top Bottom