Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Nyie Nida ni WA hovyo sana yaani ID ya kitaifa inafitika hovyo wakati Cha mpiga kura kipo Hadi Leo hii?Mwanachama wa JamiiForums.com aliandika "Ningependa kutoa kero yangu kuhusu hali ya Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufutika kwa haraka mno, na hii ni kwa vitambulisho vinavyotolewa kipindi hiki vinapoteza maandishi kwa muda mfupi tangu vitolewe hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi..."
Kusoma zaidi alichokiandika Mdau huyo, bofya hapa ~ Vitambulisho vya NIDA havidumu, vinawahi kufutika
=========================
Baada ya andiko hilo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) nayo imetoa ufafanuzi kwa kueleza yafuatayo:
Salaam Ndg.
Tunakushauri ukiwasilishe Kitambulisho cha Taifa kinachofutika kwenye ofisi ya NDA ulikosajiliwa na ueleze changamoto husika, kisha Maafisa Usajili watakipokea na kukiwasilisha kwenye madawati stahiki ili uchapishiwe kingine bila malipo.
Aidha, Mawasiliano yalishafanyika na mkandarasi ambapo ni bachi moja ina hitilafu hivyo anagharamia uchapishaji wake wa mara ya pili ndio maana Mwananchi hapaswi kulipia chochote wala Serikali haigharimiki kwa uchapishaji wa mara ya pili.
Tafadhali epuka matapeli kwani huduma inayolipiwa ni kwa mwombaji aliyepoteza Kitambulisho na ambaye kimechakaa kwa sababu za utunzaji wake mwenyewe.
Ikumbukwe tumeshatolea ufafanuzi na elimu kwa umma mara kadhaa ikiwemo kupitia Mkutano na vyombo vya Habari Januari 21, 2025 na tarehe 14 Aprili, 2025.
Vilevile kupitia vipindi mbalimbali vya redio, televisheni na kwenye Mitandao ya Kijamii ya NIDA na Wadau kwa ujumla wake ikiwemo Jukwaa hili.
Pamoja na hayo tutumie fursa hii kuwakumbusha Wananchi wote kuhakikisha wanarejesha vitambulisho vilivyofutika kwenye ofisi za Usajili za NIDA, wilayani bila kulipia chochote na pindi uchapishaji wa vitambulisho vyao unapokamilika, wanatumiwa SMS ya kuwajulisha wafike katika ofisi walikosajiliwa kuvichukua,
Tukushukuru kwa Maoni yako, Kazi inaendelea!
Mwanachama wa JamiiForums.com aliandika "Ningependa kutoa kero yangu kuhusu hali ya Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufutika kwa haraka mno, na hii ni kwa vitambulisho vinavyotolewa kipindi hiki vinapoteza maandishi kwa muda mfupi tangu vitolewe hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi..."
Kusoma zaidi alichokiandika Mdau huyo, bofya hapa ~ Vitambulisho vya NIDA havidumu, vinawahi kufutika
=========================
Baada ya andiko hilo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) nayo imetoa ufafanuzi kwa kueleza yafuatayo:
Salaam Ndg.
Tunakushauri ukiwasilishe Kitambulisho cha Taifa kinachofutika kwenye ofisi ya NDA ulikosajiliwa na ueleze changamoto husika, kisha Maafisa Usajili watakipokea na kukiwasilisha kwenye madawati stahiki ili uchapishiwe kingine bila malipo.
Aidha, Mawasiliano yalishafanyika na mkandarasi ambapo ni bachi moja ina hitilafu hivyo anagharamia uchapishaji wake wa mara ya pili ndio maana Mwananchi hapaswi kulipia chochote wala Serikali haigharimiki kwa uchapishaji wa mara ya pili.
Tafadhali epuka matapeli kwani huduma inayolipiwa ni kwa mwombaji aliyepoteza Kitambulisho na ambaye kimechakaa kwa sababu za utunzaji wake mwenyewe.
Ikumbukwe tumeshatolea ufafanuzi na elimu kwa umma mara kadhaa ikiwemo kupitia Mkutano na vyombo vya Habari Januari 21, 2025 na tarehe 14 Aprili, 2025.
Vilevile kupitia vipindi mbalimbali vya redio, televisheni na kwenye Mitandao ya Kijamii ya NIDA na Wadau kwa ujumla wake ikiwemo Jukwaa hili.
Pamoja na hayo tutumie fursa hii kuwakumbusha Wananchi wote kuhakikisha wanarejesha vitambulisho vilivyofutika kwenye ofisi za Usajili za NIDA, wilayani bila kulipia chochote na pindi uchapishaji wa vitambulisho vyao unapokamilika, wanatumiwa SMS ya kuwajulisha wafike katika ofisi walikosajiliwa kuvichukua,
Tukushukuru kwa Maoni yako, Kazi inaendelea!
Aibu kubwa kwa TAIFAHii ni aibu sana, kweli taifa linaendeshwa kwa upigaji tu.
Kadi ya mpiga kura kina zaidi ya miaka mitano lakini iko imara tofauti na hizi NIDA hata mwaka mmoja haujaisha tayari imefutika.
Leo tunaambiwa watachapisha upya lakini ni usumbufu tu hakuna cha maana. Hizo gharama za kuanza kufuatilia watatoa wao? Watu wengine wapo vijijini na NIDA zimefutika.
Ipo siku watajibu haya madudu wanayotufanyia kwa makusudi.
Cha kura ni tofauti na cha Uraia Mkuu...Uraia ni kitu nyeti sanaKuna Watu wanavitambulisho vya Nida lakini namba imefungiwa au kuna mtu ana namba lakini imefunguliwa Imesababisha Kero Kubwa sana Kwa wananchi coz mtu anashindwa kufanya mambo yake! Kwa mfano mtu amepoteza simu au imeibiwa akienda kurenew line inakataa coz namba ya Nida imefungiwa ni Changamoto kubwa sana! Ushauri wangu wasingefungia namba wangeendelea kuhamasisha wananchi wakachukue vitambulisho vyao! Pia Warahisishe huduma mtu akienda kujiandikisha apewe apo apo sio asubiri ana subiri nini sasa? Mbona cha Kura anapewa Hapo Hapo??
Yaani ni mambo ya ajabu sana, mtu alijisajilia Mwanza sada kahamia Mbeya kwahiyo atoke mbeya akavhapishe kitambulisho mwanza akili gani hii sijui harafu cha ajabu wanaongra ni watu watima kabisa na akili zao na degree zao na tai zao , jinsi gani hawapo kabisa kwa kuwasaidia wananchi, the government that doesn't even think of the live of his people , shame on you.Kwa nini isiwe kwenye ofisi yoyote ya NIDA iliyokaribu na mteja badala ya kwenda alikojisajilia?
Kuna mtu anaishi Ihusi-Bariadi lakini kajisajilia Matemanga-Tunduru.