NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kusitisha matumizi ya namba za utambulisho kwa wale waliokaidi kuchukua vitambulisho vyao.

Tangazo hilo linakuja ikiwa zimesalia siku 15 kufikia ukomo wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, la kusambaza vitambulisho milioni 1.2 vilivyotengenezwa na mamlaka hiyo, ambapo vitambulisho hivyo bado havijachukuliwa na wenyewe.
1737109813730.png

Januari 13, 2025, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Waziri Bashungwa alieleza kuwa tangu atoe agizo hilo, vitambulisho 400,000 kati ya vile vilivyokuwa vimekaa ofisini kwa muda mrefu vilitolewa kwa wananchi.

Soma, Pia: Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Nida leo Ijumaa, Januari 17, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo James Kaji ilieleza wale wote ambao hawajajitokeza kuchukua vitambulisho vyao na watakaopokea ujumbe mfupi wa maandishi katika simu zao, wanatakiwa kufika katika ofisi za NIDA za wilaya walizojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao.

“Watakaoshindwa kufanya hivyo, matumizi ya namba yao ya utambulisho wa taifa (NIN) yatasitishwa baada ya mwezi mmoja tangu kupokea ujumbe huo,” imeeleza barua hiyo.
1737109625162.png
 
NIDA wanakurupusha wananchi, kuna wengine walijiandikisha mbali mikoani na walihama bila kuondoka na vitambulisho hivyo kwani wakati wanahama vilikuwa bado havijatoka. Watoe muda mrefu angalau miezi mitatu wananchi wafanye follow up kufuatilia vitambulisho vyao huko mbali kabla hawajasitisha matumizi ya namba hizo
 
Kitambulisho ni changu sasa unafuta usajili simply sijakichukua ilimradi umenisajili na namba umenipa huu si upuuzi?

Nadhani wangesema usipochukua ndani ya huo muda wanavirudisha wilayani au mkoani hivyo utalazimika kuvifuata huko na itakugharimu kiasi fulani sababu ya usumbufu.
 
Good point.
 
Snapinst.app_474059579_2426492384371613_4965427721466465219_n_1080.jpg

Back
Top Bottom